Na Francis Godwin Blog
WANANCHI
wa Ludewa mkoani Njombe wamempongeza Rais Dr Jakaya Kikwete kwa
hatua yake ya kuwashirikisha wananchi wa maeneo husika katika suala
la utatuzi wa mgogoro wa mpaka kati ya Tanzania na Malawi
Hatua
ya wananchi hao kumpongeza Rais Dr Kikwete imekuja huku ikiwa
ni siku tatu zimepita toka mbunge wao wa jimbo la Ludewa Deo
Filikunjombe ,mbunge wa jimbo la Kyela Dk.
Harrison Mwakyembe na mbunge wa jimbo la Mbinga Magharibi John
Komba kurejea nchini kutoka Malawi katika kikao cha usuluhishi wa
mgogoro wa mpaka kati ya Malawi na Tanzania Wakizungumza
na mwandishi wa habari hizi wananchi hao akiwemo Yohana Haule
walisema kuwa hatua ya Rais Kikwete kutumia wananchi wenye
kushughulikia suala hilo ni hatua ya kupongezwa kwani wabunge hao
ni wawakilishi wa wananchi hivyo kila kinachoendelea kitawafikia
mapema wananchi wa maeneo ya mpakani Malawi na Tanzania. Haule
alisema kuwa imani na matumani ya wana Ludewa ni kuona mbunge wao
amewawakilisha katika suala hilo na kuwa hawana shaka na
uwakilishi wake na wanaamini watapewa mrejesho wa kila
kinachoendelea katika suala hilo. Hivyo
alisema kwa sasa hofu ambayo awali wananchi wa kando ya ziwa
Nyasa walikuwa nayo juu ya mgogoro huo wa mpaka kati ya Tanzania na
Malawi imeanza kutoweka kutokana na mbunge wao Filikunjombe
kuzunguka maeneo yote ya Mwambao na kufanya mikutano na kuwaondoa
hofu juu ya hilo. Huku
Sarah Haule mbali ya kumpongeza Rais Kikwete kwa hatua hiyo
pia alimpongeza mbunge Filikunjombe kwa jitihada mbali mbali za
kuwaletea maendeleo wananchi wa Ludewa huku akimtaka mbunge huyo
kuendelea na msimamo wake katika kuwawakilishi wana Ludewa bungeni
0 comments :
Post a Comment