Kocha David Moyes na kocha mchezaji wa klabu ya Manchester United Ryan Giggs wameripotiwa kutoelewana.
Imeripotiwa
kwamba gwiji huyo wa United aligoma kuhudhuria mkutano wa benchi la
ufundi na alimwambia kocha mwenzie msaidizi Phil Neville hakukuwa na
haja ya kwenda kwenye mkutano huo kwa sababu kocha mkuu wa timu David
Moyes hasikilizi ushauri wake.Kwa mujibu wa jarida lenye ukaribu na
klabu ya Manchester United, Fanzine, Moyes ameripotiwa kutokuwa na
mahusiano mazuri ya kiungo Micheal Carrick kutokana na mbinu
anazomuelekeza akimlazimisha mchezaji huyo kuangalia video za kiungo wa
Everton Leon Osman ili aige namna anavyocheza, jambo ambalo Carrick
amewaambia jamaa zake wa karibu linamkera. Pia Rio Ferdinand nae
inasemekana ametofautiana na Moyes juu kuiga mbinu za beki wa Everton
Phil Jagielka.
(J.G)
0 comments :
Post a Comment