CP
Mussa Ali Mussa, akitoa maagizo kwa Wakaguzi wa Polisi wanaoshiriki
katika mafunzo ya Miundombinu ya Maadili na mikakati ya kudhibiti rushwa
yanayofanyika mjini Dodoma.
Wakaguzi
wa Polisi kutoka mikoa mbalimbali nchini wanaoshiriki mafunzo ya
miundombinu ya maadili na mikakati ya kupambana na vitendo vya rushwa
wakimsikiliza Kamishna wa Polisi Jamii nchini CP. Mussa Ali Mussa,
wakati akitoa mada juu ya umuhim wa Polisi Jamii.
Afisa
Habari Mkuu wa Jeshi la Polisi Zanzibar Inspekta Mohammed Mhina,
katikati akiwaelekeza jambo waandishi wa Habari wa Jeshi la Polisi
walioshiriki katika mafunzo ya Miundombinu ya Maadili na mikakati ya
kupambana na rushwa. kushoto ni Insp. Dickison Gibeshi na kulia ni Sgt
Shabani Msangi,
………………………………………………………………………………..
Na Mohammed Mhina, wa Jeshi la Polisi -Dodoma
DODOMA,
JUMAPILI MACHI 16, 2014. Maafisa na Askari Polisi hapa nchini,
wametakiwa badili tabia zao kwa kujiepusha na vitendo vya kudai na
kupokea rushwa kutoka kwa watu wenye Matatizo yanayohitaji huduma za
kipolisi.
Hayo
yameelezwa na Mkuu wa Kitengo Ufuatiliaji na Tathimini cha Jeshi la
Polisi nchini, Naibu Kamishna (DCP) Mpinga Gyumi, wakati akitoa mada kwa
washiriki wa Mafunzo ya kuimarisha Miundombinu ya Maadili na mapambano
dhidi ya Rushwa yanayotolewa kwa Wakuu wa Polisi wa Tarafa na Majimbo
yanayofanyika mjini Dodoma.
DCP
Gyumi, ameonya kuwa Jeshi la Polisi halitamvumilia Afisa ama Askari
yeyotw atakayekwenda kinyume na maadili ya Jeshi hilo jambo ambalo
amesema limekuwa likipakwa matope.
Akikariri
baadhi ya vifungu vilivyomo kwenye kitabu cha miongozo ya Jeshi la
Polisi nchini Police General Order (PGO), amesema kitabu hicho kimetoa
makatazo kwa Askari Polisi wa vyeo mbalimbali na kutoa maelekezo mazuri
yanayofaa kufuatwa na kila Askari Polisi.
DCP Gyumi
pia amewakumbusha Maispekta hao pamoja na Maafisa wa ngazi ya juu wa
Jeshi hilo kujiepusha na vitendo vya kupokea zawadi kwani kwa kufanya
hivyo ni sawa na kuhalalisha rushwa.
Amesema
rushwa imekua ikipunguza heshma na uadilifu kwa mtumishi na hivyo
kumfanya kushindwa kuheshimu sheria, kanuni, taratibu na kuwafanya
baadhi ya watumishi kujilimbikizia mali kwa njia zisizo halali, wizi na
ubadhirifu wa mali ya umma.
Amewaonya
wale wote wanaojihusisha na matumizi mabaya ya mali za umma kama vile
magari, kompyuta, mashine na vitendeakazi vingine kuacha kufanya hivyo
kwani matokeo yake ni kuitia serikali hasara.
Amewataka
Maafisa na Askari wa ngazi zote kuwa wasafi mbele ya Jamii hali
itakayilifanya Jeshi la Polisi kuwa kimbilio la wanyonge na sio
kukimbiwa. “ Nawaombeni kila mmoja wenu kutimiza wajibu wake na kuzaliwa
upya hata kama anadhani ameshindikana”. Alisema DCP Byatao.
Naye
Kamishna wa Polisi Jamii nchini CP Mussa Ali Mussa, amewataka Mainspekta
hao kuhakikisha kuwa wanaondokana na vitendo vya kudai na kupokea
rushwa ili wawe mfano bora kwa jamii na Askari waliochini yao.
Awali
Mkuu wa Kitengo cha Maadili na Nidhamu cha Jeshi la Polisi nchini SACP
Patrick Byatao, alisema hadi sasa, zaidi ya Polisi 1,100 wakiwemo
Maafisa Wanadhimu wa Polisi wa mikoa, Wakuu wa Upelelezi wa wilaya na wa
Usalama Barabarani hapa nchini, wameshanufaika na mafunzo hayo
yanayofadhiliwa na Shirika la Misaada la Maendeleo la nchini Uingereza
(DFID)
0 comments :
Post a Comment