Mgombea ubunge wa jimbo la Chalinze kupitia Chama cha Mapinduzi Ndugu Ridhiwani
Kikwete akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Ubena Zomozi katika mkutano
wa kampeni uliofanyika kijijini hapo huku mvua kubwa ikinyesha na
kuwafanya wananchi hao kugeuza viti vyao na kuvifanya miamvuli ya
kujikinga na mvua hiyo, kutokana na kukunwa na hotuba ya mgombea ubunge
huyo ambaye alizungumzia matatizo mbalimbali yakiwemo masuala ya maji,
umeme, elimu afya na mengine kadhaa na kuahidi kuyafanyia kazi na
kuyatekeleza kwa kufuata ilani ya uchaguzi ya chama cha mapinduzi CCM,
Uchaguzi wa jimbo la Chalinze unafanyika Aprili 6 jumapili kuziba pengo
la aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo marehemu Saidi Bwanamdogo aliyefariki
dunia hivi karibuni.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-CHALINZE) Baadhi ya wananchi wakiwa wamejikinga na mvua kwa kutumia viti vyaoBaadhi
ya wananchi wakiwa wamejikinga na mvua kwa kutumia viti vyao wakati
wakifuatilia hotuba ya Ridhiwani Kikwete alipowaomba kura katika kijiji
cha Ubena Zomozi leo.Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wa pili kutoka kulia pamoja na
viongozi wa kijiji hicho wakifuatilia hotuba ya mgombea ubunge wa jimbo
la Chalinze Ndugu Ridhiwani Kikwete huku wakiwa wamesimama kutokana na
mvua iliyokuwa ikinyesha wakati wa mkutano huo.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimuombea kura Ridhiwani Kikwete
huku mvua ikinyesha ambapo aliwaambia wananchi hao wamchague mgombea
huyo kwakuwa Chama cha Mapinduzi kimemuamini na kumsimamisha katika
kuomba nafasi hiyo na kinaamini kwamba anatosha.Umati wa tu ukiwa katika mkutano huo kabla ya mvua kunyesha.Kikundi cha ngoma kikitumuiza katika mkutano huo.Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimsikiliza Ridhiwani Kikwete
wakati walipokuwa wakiwasili katika eneo la mkutano kulia ni Mzee Kazidi
Meneja kampeni wa mgombea huyo ambaye pia ni Katibu wa CCM mkoa wa
Kilimanjaro.Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana katikati Ridhiwani Kikwete kulia
nia Mwenyekiti wa kata ya Fukayose Olinjurie Marigwa wakiwasili katika
eneo la mkutano Ubena Zomozi.Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimsikiliza Dr. Shukuru Kawambwa
mbunge wa jimbo la Bagamoyo na Waziri wa Elimu na mafunzo ya ufundi
katikati ni Mwenyekiti wa tawi la Msolwa Khalfan Changali. Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimsikiliza Ridhiwani Kikwete wakati mkutano huo wa kampeni ulipokuwa ukiendelea.Dr. Shukuru Kawambwa mbunge wa jimbo la Bagamoyo na Waziri wa Elimu na mafunzo ya ufundi akimuombea kura Ridhiwani KikweteJoseph Msukuma Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Geita akimuombea kura Ridhiwani Kikwete.-
Blogger Comment
-
Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments :
Post a Comment