RATIBA
[Saa za Bongo]
Jumanne Machi 25
2245 Arsenal v Swansea
2245 Man Utd v Man City
2245 Newcastle v Everton
++++++++++++++++++++
FA,
Chama cha Soka England, kimethibitisha kuwa Wachezaji wa Arsenal,
Kieran Gibbs na Alex Oxlade-Chamberlain, wanaruhusiwa kucheza Mechi ya
Ligi Kuu England ya Jumanne Usiku wakati Timu yao itakapokutana na
Swansea City Uwanja wa Emirates.
Fulbeki Gibbs alionyeshwa Kadi Nyekundu
kimakosa na Refa Andre Marriner Jumamosi wakati Arsenal inabamizwa Bao
6-0 Uwanjani Stamford Bridge wakati alietenda kosa la kushika Mpira kwa
mkono alikuwa ni Oxlade-Chamberlain.
Usiku huu, FA imethibitisha kuwa Kadi Nyekundu iliondolewa kwa Gibbs na kuhamishiwa kwa Oxlade-Chamberlain.
Lakini Arsenal wakakata Rufaa kupinga
Adhabu hiyo kwa Oxlade-Chamberlain wakidai Mchezaji huyo hakuwa akizuia
kufungwa kwa Goli kwa vile Mpira huo uliopigwa na Eden Hazard ulikuwa
ukitoka nje.
Taarifa ya FA ilisema: “Jopo Huru la
Sheria limesikiliza Rufaa mbili za Arsenal, moja ikiwa ni kumkosea
Mtuhumiwa na pili la kupewa Kadi Nyekundu isiyostahili, yote yakihusu
Mechi ya Jumamosi na Chelsea huko Stamford Bridge. Kuhusu Kadi Nyekundu
kwa Gibbs, Jopo limeona Kadi hiyo ni makosa na ikahamishiwa kwa Mchezaji
mwenzake Alex Oxlade-Chamberlain. Baada ya hapo, Jopo likapitia madai
ya Arsenal kwamba Oxlade-Chamberlain hakustahili Kadi Nyekundu na
kukubaliana nao. Hivyo, Oxlade-Chamberlain hatatumikia Adhabu yeyote.”
SOURCE:SOKAINBONGO
0 comments :
Post a Comment