-->

KOCHA WA YANGA AWEKA SHARTI GUMU KWA MANJII ILI AENDELEE KUFUNDISHA

SAM_2259KOCHA Mkuu wa Yanga Hans Pluijm amesema yupo tayari kuongeza mkataba lakini akamtaka mwenyekiti wa klabu hiyo Yusuf Manji kufuta mpango wake wa kutogombea tena kwenye uchaguzi ujao.
Akizungumza na Mwanaspoti Pluijm alisema awali alikuwa na mashaka juu ya uimara wa Yanga  na ndani ya miezi mitatu aliyodumu klabuni hapo ameona uimara wa timu na sasa akili yake inaganga yajayo.
Alisema Manji amekuwa msaada mkubwa katika kuiongoza Yanga kupata mafanikio: “Nimefikiria kwa kina nimeona niendelee kuwa hapa kwa muda zaidi, nataka kuongeza mafanikio ambayo tumeyaanza miezi mitatu iliyopita, uamuzi wangu umetokana na mipango inayoridhisha ya timu hii hasa uongozi.”
“Kuhusu kuondoka kwa Manji sidhani kama anaweza kufanya uamuzi kama huo, ni kati ya watu ambao nguvu yao inahitajika katika timu, amekuwa msaada mkubwa kuiboresha timu, Manji hahitajiki kwa Yanga pekee bali hata katika maendeleo ya soka Tanzania, nafikiri atabadili mawazo yake haraka,”alisema kocha huyo ambaye uongozi umethibitisha kwamba utamuongezea mkataba.
Pluijm amewaambia nyota wake kwamba kazi yao ni kuhakikisha wanashinda michezo yao  iliyosalia lakini hataki kufikiria matokeo ya timu zingine.
SOURCE: MWANASPOTI
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment