Akizungumza, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Sekretarieti ya Ajira, Riziki Abraham, alisema katika kupokea maombi ya kazi, wamebaini udanganyifu wa hali juu wa vyeti kwa wanaomba kutoka makazini na wahitimu. (J.G)
"Tangu miaka minne iliyopita hadi
sasa, Sekretarieti ya Ajira imebaini kuwapo kwa matumizi ya vyeti feki
wakati wa kuomba kazi, barua nyingi zimeonekana kuambatanishwa na nakala
feki," alisema.
Aliongeza: "Ni jambo la kusikitisha kuona mtu anatumia vyeti ambavyo si vyake kwa lengo la kujipatia kazi kiudanganyifu au wengine wanajaribu kuongeza vigezo ambavyo hana kwa kazi anayoomba ambapo husababishwa kutoitwa kwenye usaili,", alisema.
Abraham alisema kuwa ofisi ya Sekretarieti ya Ajira katika utumishi wa umma inajipanga kutoa elimu kwa wahitimu na wadau mbalimbali wa elimu katika kuzitatua changamoto hizo.
Aliongeza kuwa sekretarieti hiyo katika kukabiliana na changamoto hizo wanatarajia kuhama katika mfumo wa analojia na kwenda dijitali ambapo wahitimu na walio makazini watatuma maombi kwa njia ya kielektroniki.

0 comments :
Post a Comment