-->

YANUKOVUYCH ASISITIZA KWAMBA YEYE BADO NI KIONGOZI WA NCHI YA UKRAINE

UKRAIN_26c20.jpg
Kiongozi wa Ukraine aliyetolewa madarakani Viktor Yanukovych aliwalaumu wapinzani wake Jumanne kwa hatua za Crimea kujiondoa Ukraine na kusema yeye bado ni rais halali wa nchi hiyo.
Bwana Yanukovych alizungumza kwa mara ya pili mbele ya umma kutoka uhamishoni Rostov –on – Don , huko Russia alipokimbilia tangu mwezi uliopita kufuatia maandamano ya kupinga serikali nchini mwake.
Alishutumu utawala ulioko madarakani kwa muda huko Ukraine akisema kuwa ni wenye msimamo mkali na kushutumu uchaguzi uliopangwa kufanyika Mei 25 kuwa si halali na unakiuka sheria.
Bw.Yanukovych pia aliishutumu Marekani na msaada wake wa dola bilioni moja kwa serikali ya muda akisema serikali ya Marekani haina haki ya "kuwapa fedha majambazi."
Wakati huo huo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa Laurent Fabius aliiambia Inter radio ya Ufaransa kwamba nchi za magharibi zinaweza kuiwekea Russia vikwazo haraka iwezekanavyo hata ikibidi mapema wiki hii ikiwa Moscow haitafuata mapendekezo ya kupelekea utulivu huko Crimea.
Chanzo: VOA
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment