UPUNGUFU WA MADINI JOTO MWILINI (GOITA)
Baada ya somo mwanafunzi ajue mambo yafuatayo:-
1. Maana ya upungufu wa madini joto mwilini
2. Dalili za upungufu wa madini joto mwilini
3. Sababu za kupata upungufu wa madini joto mwilini
4. Jinsi ya kuzuia upungufu wa madini joto mwilini na
5. Matibabu ya upungufu wa madini joto mwilini.
1. Maana ya upungufu wa madini joto mwilini.
Huu ni uvimbe usio wa kawaida katika kikoromeo(Thyroid Gland) ambao hutokea mbele ya shingo)
2. Dalili za upungufu wa madini joto mwilini (Goita)
i. Uvimbe mbele ya shingo
ii. Mama wajawazito kuharibu mimba
iii. Kudumaa mwili na akili
iv. Mtoto kufia tumboni
v. Kuzaliwa mtoto njiti (uzito pungufu au premature)
vi. Kutetemeka na kuwa na wasiwasi.
vii. Macho kutoka nje
3. Sababu za kupata upungufu wa madini joto mwilini.
i. Kupungua kwa IODINE katika chakula
ii. Lishe duni
4. Jinsi ya kuzuia upungufu wa madini joto mwilini
i. Kutumia chumvi yenye Iodine (ayodini) hasa ile ya baharini
ii. Kutumia vyakula vyenye Iodine(ayodini) kwa wingi kama vile dagaa, maziwa nk.
iii. Kutoa elimu ya afya kwa jamii kuhusu umuhimu wa lishe bora na
iv. Kumpeleka mgonjwa hospitali iwapo ameshaanza dalili
5. Matibabu ya upungufu wa madini joto mwilini
i. Mgonjwa ataagiziwa dawa ya Iodine na daktari
ii. Tumia dawa kama utakavyoagizwa na
iii. Operesheni itakayofanyika kama tezi imekuwa kubwa na athari zake zimeonekana
-
Blogger Comment
-
Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments :
Post a Comment