-->

ASKARI WA UMOJA WA MATAIFA WAPAMBANA VIKALI NA ANT-BARAKA HUKO AFRIKA YA KATI


skari wa kimataifa walioko Bangui, mji mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati jana walipambana vikali na wanamgambo wa Kikristo wa Anti Balaka.
Mapigano hayo yalishirikisha askari wa kimataifa kutoka Burundi wanaojaribu kuzuia mashambulizi ya wanamgambo hao dhidi ya Waislamu huku helikopta za jeshi la Ufaransa zikifanya doria katika anga ya baadhi ya vitongoji vya mji wa Bangui.
Msemaji wa Waislamu wa kitongoji kimoja cha Bangui Othman Abakar amesema kuwa Waislamu 8 wamejeruhiwa katika mapigano hayo. Abakar ameongeza kuwa wanamgambo wa kundi la Anti Balaka wanafanya jitihada za kushambulia msikiti mkuu wa Bangui.
Mamia ya Waislamu wameuawa na maelfu ya wengine kujeruhiwa katika mashambulizi yanayoendelea kufanywa na wanamgambo wa Kikristo wa Anti Balaka katika Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Shirika la Kutetea Haki za Binadamu la Human Rights Watch limelaani vikali mauaji yanayofanywa na wanamgambo wa Anti-Balaka dhidi ya Waislamu na kusisitiza kuwa hali hiyo haiwezi kuvumiliwa.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment