Kikosi cha Barcelona kilichoanza.
FC Barcelona vs Manchester City,
Mtanange wa kipindi cha kwanza unamalizika wa dakika 45 wakiwa bado 0-0,
Hakuna cha Barca wa City, Barcelona wakijaribu mara kwa mara kuingia
kwenye eneo la hatari la City bila kufunga, Neymar na Messi wakikosa
mabao. Wao
City nao wamejaribu kuingia lakini shuti lililopigwa na Nasri lilidakwa
na Kipa wa Barca. Kumbuka katika Mtanange wa kwanza walitoka 2-0 huko
Etihad na sasa Man City wanataka kupindua kipigo hicho cha bao hizo
mbili na kuwatupa nje Barcelona kwenye uwanja wao Nou Camp.Messi na Aguero wakioneshana ubabe!
Kipindi cha pili dakika ya 67 Lionel
Messi akaipachikia bao Barca baada ya mabeki wa City kujichanganya.
Lescott akituliza mpira bila umakini na hatimae Messi kuuchukua na
kutupia nyavuni. Dakika ya 78 Mchezaji wa City Pablo Zabaleta anaonshwa
kadi ya njano na nyekundu na kutolewa nje ya uwanja baada ya kufanya
ndivyo sivyo na Mwamuzi S. Lannoy kumtoa nje. Dakika ya 80 Barca
walifanya mabadiliko Neymar alitoka na nafasi yake ilichukuliwa na
Alexis Sánchez. Dakika za lala salama dakika ya 89 kona ilipigwa na
hatimae Vincent Kompany akasawazisha bao kwa kufanya 1-1(Agg.3-1) na
hapo hapo kwenye dakika za majeruhi dakika za nyongeza Barcelona
walifanya mashambulizi na kupachika bao la pili kwa kufanya 2-1 (Agg.
4-1) Bao lililofungwa na Daniel Alves akipewa pasi safi na Andrés
Iniesta Luján ndani ya box na kuachia shuti kali hadi ndani ya lango la
City na mpira kumalizika. Ushindi huu wa Barca unawaondosha City nje ya
michuano hii ya Uefa kwenye hatua ya 16 bora, Huku Barca wakisonga
mbele kwenye hatua ya robo fainali.Kocha wa City kautazamia kwa mashabikiYaya Toure na pique wakichuana vikali Silva akiupoza mpiraIniesta mbele ya Vicent KompanyHapa hukatizi ndugu yangu ....hapa ni Nou Camp!Chupu chupu hapa Vicent Kompany kidogo awapige bao la kichwa..katika kipindi cha kwanza.Kidogo!!Lescott akipitwa na Lionel MessiNeymar baada ya kukosa bao la wazi hapa!!Neymar akionekana kuumia kukosa bao!Mtu kati...Daniel Alves akichuana hapa ...nivute ni kuvute na David SilvaNeymar akiendesha...Utakubali tuu!Messi na LescottPicha mbali .....kaa pembeni!!Nani fundi hapa!Neymar kwenye patashika na wachezaji wa City!Hoi!!! msaidizi wa kocha wa City Ruben Cousillas Unakosa!!tutajutia baadae......Benchi halikukalika!!!Kocha
wa England Roy Hodgson nae yupo Spain live kuangalia kipute cha vijana
wake wanaokipiga katika timu ya Taifa, Na hapa alikuwa akiteta jambo na
kupeana salama na Manuel Pellegrini wa City pamoja na viongozi wengine
kwenye uwanja wa Nou Camp.
VIKOSI:
Barcelona: Valdes, Dani Alves, Pique, Mascherano, Jordi Alba, Xavi, Busquets, Iniesta, Messi, Fabregas, Neymar.
Subs: Pinto, Pedro, Alexis, Bartra, Song, Adriano, Sergi Roberto.
Manchester City: Hart, Zabaleta, Kompany, Lescott, Kolarov, Silva, Fernandinho, Milner, Nasri, Toure, Aguero.
Subs: Pantilimon, Negredo, Dzeko, Javi Garcia, Jesus Navas, Clichy, Boyata.
Referee: Stephane Lannoy (France)
-
Blogger Comment
-
Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments :
Post a Comment