-->

MCHINA JELA MIAKA 2O KWA KUKUTWA NA MENO YA TEMBO

 Kamanda Kanda Maalum, Seleman Kova akiwa ameshika meno ya tembo.
Mahakama  ya Hakimu Mkazi Kisutu, imemhukumu raia wa China, Yu Bo (45), kulipa faini ya Shilingi  bilioni tisa au kwenda jela miaka 20 baada ya kukiri kukutwa na nyara za serikali.
Yu, alikamatwa akiwa na kilo 303 za nyara hizo ikiwamo ngozi za vinyonga wawili vyote vikiwa na thamani ya Sh. milioni 975 mali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Hukumu hiyo ilitolewa jana na Hakimu Mkazi, Devota Kisoka, baada ya upande wa Jamhuri kumsomea mshtakiwa mashitaka na kukiri.
Alisema baada ya mshtakiwa kukiri makosa yake, mahakama imemtia hatiani na kumhukumu kulipa faini ya Shilingi bilioni tisa na akishindwa aende jela miaka 20.


Hata hivyo, hadi NIPASHE inaondoka mahakamani hapo jana saa 9:00 alasiri Yu alikuwa hajafanikiwa kulipa faini hiyo.
Kabla ya hukumu hiyo kusomwa, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Faraja Nchimbi, alidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na alimkumbusha mshtakiwa mashitaka yake.
Nchimbi alidai kuwa Desemba 30, mwaka 2013, katika Bandari ya Dar es Salaam, mshtakiwa alikutwa na nyara hizo bila kuwa na leseni ya Mkurugenzi wa Wanyamapori.
Alidai kuwa mshtakiwa alikutwa akiwa na vipande 81 vya pembe za ndovu ambazo zimetokana na kuwaua tembo 40 zenye thamani ya Sh. 975,076,350 na ngozi mbili za vinyonga wawili zenye thamani ya Sh. 3,044,140 vyote vikiwa na jumla ya thamani ya Sh. 978,120,490 mali ya Serikali ya Tanzania.
Mshtakiwa baada ya kusomewa maelezo hayo alikiri na mahakama ikamhuku adhabu hiyo.
CHANZO: NIPASHE
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment