-->

NAIBU WA WAZIRI WA FEDHA MWIGULU NCHEMBA AFANYA SAFARI KWENDA UJERUMANI NA UFARANSA

 
NAIBU WAZIRI WA FEDHA MH:MWIGULU LAMECK NCHEMBA ZIARANI NCHINI UFARANSA NA UJERUMANI KUHUDHURIA MKUTANO WA ACP NA DEVELOPMENT COOPERATION FORUM
 
Naibu Waziri wa Fedha Mh.Mwigulu Lameck Nchemba ameanza ziara yake ya Kikazi Nchini Ufaransa kwa Muda wa Siku mbili (Tar.18 na 19/03/2014) atakapo hudhuria Mkutano wa Umoja wa Nchi za Africa,Caribbean na Pacific.Mkutano huo ni Miongoni mwa Mikutano ilinayofanyika Kila Mwaka ya Umoja huo.Kwenye Mkutano huo Mh.Mwigulu Nchemba natarajia Kushiriki Mjadiliano ya namna ya Kuzijengea Uwezo madhubuti Nchi zinazoendelea katika Maswala ya Biashara na Uwekezaji.Pia watafanya tathimini ya Utekelezaji wa Mikakati ya Maendeleo waliokuwa Wamejiwekea Mwaka 2013.
Baada ya Ufaransa,Mh.Mwigulu Nchemba ataelekea Nchini Ujerumani kuhudhuria Mkutano wa Jukwaa la Ushirikiano wa Maendeleo (Development Cooperation Forum),Mkutano utakao husisha Nchi zilizoendelea,Zinazoendelea na Taasisi Kubwa za Kifedha na Maendeleo Duniani.
Katika Mkutano huu wa Ujerumani,Washiriki watajadiliana namna Misaada inayotolewa inavyotumika Kwenye Shuguli zilizolengwa za Maendeleo na Vile Vile Utekelezaji wa ahadi za Utoaji wa Misaada kutoka Nchi zilizoendelea katika hali ya Uwazi.
Naibu Waziri wa Fedha atakuwepo Ujerumani kwa Muda wa Siku mbili(Tar.20 na 21/03/2014).
Mungu Ibariki Tanzania.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment