Wachezaji wa Young Africans wakiwa mazoezini leo jioni katika Uwanja wa El Max Alexandria
Wawakilishi pekee wa Tanzania kwenye
mashindano ya Klabu Bingwa Barani Afrika Young Africans Sports Club leo
usiku wamefanya mazoezi ya mwisho katika Uwanja wa El Max Haras El
Hodod jijini Alexandria tayari kwa mchezo marudiano kati ya mabingwa
watetezi Al Ahly.
Kikosi cha Young Africans kilichowasili
mchana wa leo jijni Alexandria kikitokea jijini Cairo kimefanya mazoezi
katika uwanja huo utakaotumika kwa ajili ya mchezo wa kesho, huku morali
ya wachezaji kuelekea mchezo huo ikiwa ni ya hali ya juu sana.
Wachezaji 20 waliopo Alexandria wamefanya
mazoezi chini ya makocha Hans Van der Pluijm, Charles Mkwasa pamoja na
kocha wa makipa Juma Pondamali anayewanoa magolikipa na kuhakikisha
wanaendelea kuwa fit kwa ajili ya mchezo huo.
Kesho kikosi cha mdachi Hans kitaingia
uwanjani kikiwa na kumbukumbu ya ushindi wa bao 1-0 lililofungwa na
Nadir Haroub "Cannavaro" katika mchezo uliofanyika mwishoni mwa wiki
jijini Dar es salaam na kuhakikisha kinapata ushindi na kusonga mbele
katika hatua inayofuata.
Kuelekea mchezo wa kesho ambao utaonyesha
na televison zaidi ya 8 za nchini Misri, maandalizi yote yameshakamlika
na katika kikao cha maandalizi ya mechi kamisaa ameendelea kusisitiza
kuwa mchezo hautakua na mashabiki wa aina yoyote.
Wachezaji waliopo nchini Misri na kufanya mazoezi ya mwisho leo jioni ni"
Magolikipa: All Mustafa "Barthez", Juma Kaseja, Deogratias Munish "Dida"
Walinzi: Juma Abdul, Mbuyu Twite, Oscar Joshua, David Luhende, Kelvin Yondani "Cotton", Nadir Haroub "Cannavaro"
Viungo: Haruna Niyonzima, Saimon Msuva, Athuman Idd "Chuji", Frank Domayo "Chumvi", Nizar Khalfani
Washambuliaji: Mrisho Ngasa, Said Bahanuzi, Emmanuel Okwi, Hamis Kizza, Jerson Tegete na Didier Kavumbagu
Mechi itachezwa kuanzia majira ya saa
1kamili kwa saa za Misri sawa na saa 2 usiku kwa saa za Afrika
Mashariki, na kesho wapenzi, wadau na wanachama wa Young Africans
watapatiwa link ya kuweza kutazama mchezo huo moja kwa moja kwa kutumia
internet.
Mungu Ibariki Young Africans, Mungu Ibariki Tanzania
0 comments :
Post a Comment