-->

TATHMINI NA SWALI DOKEZO KUHUSU MCHEZO KUHUSU EL CLASSICO YA MADRID NA BARCA

Na Baraka Mbolembole,
Real Madrid ilitoka nyuma na kuifunga FC Barcelona kwa mabao 3-1 katika mchezo wa ligi kuu ya Hispania, La Liga. Ikicheza katika uwanja wa nyumbani, Santiago Bernabeu, mshambulizi Karimu Benzema alifunga mara mbili huku mwanasoka bora wa dunia, Cristiano Ronaldo pia akifunga kwa mkwaju wa penalti.
Real Madrid ilionekana kushtushwa na bao la mapema la mshambulizi, Neymar na safu ya mashambulizi ya wapinzani wao ilikuwa ya ‘ kutisha’. Katika makatarasi, Barca ilikuwa na wachezaji bora watatu katika safu ya mashambulizi, Neymar, Leonel Messi na Kuis Suarez ambaye alikuwa akicheza mchezo wake wa kwanza tangu mwezi Juni alipofungiwa na FIFA kwa kosa la kumng’ata meno mlinzi wa Italia, Giorgio Chiellini katika mchezo wa kombe la dunia nchini Brazil ambao ulihusisha timu za Uruguay na Italia.
Real iliingia ikiwa na ‘ hofu’ licha ya kuitandika Liverpool kwa mabao 3-0 katika uwanja wa Anfield katikati ya wiki iliyopita. Ikel Casillas alifanya kazi kubwa langoni, Segio Ramos na Pepe walikuwa wagumu katika ngome ya kati wakati Marcelo alipoweza kumzima Suarez. Ikicheza bila mchezaji ghali zaidi duniani, Real Madrid ilionekana haina tatizo kutokana na kutokuwepo kwa mshambulizi, Gareth Bale.
rooo
Isco, Luka Modric na Ton Kroos ni safu kabambe ya Real ambayo kocha ‘ mtaalamu’ Carlo Ancelotti aliinzisha dhidi ya Xavi Hernandez, Sergio Busquets na Andres Iniesta ambao walianza kwa upande wa Barcelona katika eneo la kiungo. Kroos alikuwa kiongozi, akicheza kwa nguvu huku akishambulia kwa mipira mirefu mchezaji huyo wa Ujerumani alikuwa bora sana lakini kamwe huwezi kuacha kuwasifu, Isco na Modric ambao waliivuruga Barca katikati ya uwanja.
Real ilionekana ni timu bora zaidi ya Barcelona, mlinzi Gerlad Pique ‘ alijigeuza golikipa’ pale alipodaka mpira ndani ya eneo lake la hatari . Hiyo ilikuwa ni dalili ya ubora wa Bsrca kuwa mdogo. Timu ambayo ilikuwa imefunga mabao 22 katika michezo nane iliyopita huku ikiwa haijaruhusu bao lolote ilifungwa huku Ronaldo akiwa na ‘ siku mbaya’. Mshambulizi huyo wa Ureno alipoteza nafasi takribani nne za kufunga, ingeweza kuwa siku mbaya zaidi kwa Barcelona na wameondoka Bernabeu wakishukuru kufungwa mabao 3-1.
ronaldo
Wakicheza huku wakibadilisha nafasi, C. Ronaldo, Benzema na Mcolombia, James Rodriguez walikuwa katika kiwamgo bora kiasi cha kuichanganya beki ya Barcelona ambayo ilikuwa chini ya Pique na Jeremy Mathieu, Javier Mscherano na Dan Alves. Barcelona iliruhusu goli la kwanza baada ya kucheza dakika 776. Ancelotti alifamya mabadiliko ya wachezaji wawili kutoka katika kikosi kilichocheza na Liverpool. Daniel Carvajal na Ramos walianza na kucheza kwa dakika zote 90, huku wachezaji kama Sam Khedira, Alvaro Arbeloa, Jsvier Hernandez, Aiser Illarramendi, na Raphael Varane wakiwa katika benchi. Calo alikuwa na machuguo ya kutosha kuliko mpinzami wake Luis Enrique ambaye nje alinakiwa na Pedro Rodriguez, Ivan Rakitic, Jordi Alba, Marc-Andre ter Stegen, Marco Bartra, Sergi Roberto na Munir El Haddadi.
Kwa sasa Real ipo nyuma ya Barca kwa tofauti ya pointi moja. Msimu uliopita ‘ Los Blancos’ waliongoza ligi kwa muda Fulani lakini mambo yalikuwa mabaya kuelekea michezo ya mwisho. Malengo makuu msimu uliopita ilikuwa ni timu hiyo kutwaa ‘ La Decima’ jambo ambalo limewezekana, lakini uwezo walionao sasa unaweza kuwafanya kurudisha taji la La Liga ambalo walitwaa mara ya mwidho msimu wa 2011/12. Je, Real inaweza kutwaa ubingwa wa La Liga msimu huu, ni jambo la kusubiri na kuona. Uwezo wanao.
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment