Kiungo mshambuliaji wa Yanga, Andrey Coutinho
anaonekana yuko fiti kweli, ikiwezekana mabeki wa Simba wanatakiwa kuwa makini.
Raia huyo wa Brazil amekuwa akiwapa wakati
mvumu mabeki wa Yanga na hasa wale ngangari kama Nadir Harob ‘Cannavaro’ na
Kelvin Yondani.
Pamoja na kuwa imara lakini Cannavaro na
Yondani walilazimika kufanya kazi ya ziada kumzuia.
Mara kadhaa walilazimika kumkumbatia au
kumfanyia madhambi kutokana na ujanja wake.
Mabeki wa Simba watakuwa na kazi ya kumzuia
kesho Jumamosi wakati watani hao watakapokutana.
Kocha Marcio Maximo amekuwa akimpanga ili apambane na mabeki imara kama Cannavaro na Yondani.
0 comments :
Post a Comment