LIVERPOOL imeshinda 3-2 dhidi ya Queens Park Rangers jioni ya leo katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa ugenini.
Mabao
ya Liverpool yamefungwa na Richard Dunne aliyejifunga dakika ya 67,
Philip Coutinho dakika ya 90 na Steven Caulker aliyejifunga pia dakika
hiyo hiyo ya 90.
Richard Dunne leo ameweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kujifunga mabao 10 katika historia ya Ligi Kuu ya England.
Raheem
Sterling alianza leo kwenye kikosi cha Liverpool na kocha wa England,
Roy Hodgson akamshuhudia kutokea jukwaani. Mario Balotelli alikosa bao
akiwa amebaki yeye na nyavu, baada ya kupiga juu akiwa
umbali wa mita tatu wakati huo matokeo bado yapo sare.Katika mchezo huo jumla ya magoli manne yalifungwa kuanzia dakika ya 87 yaani dakika ya 87 na 90 magoli ya QPR huku LIVER wakipata magoli dakia ya 90 na 93
yaani ilikuwa kama miujiza vile
MAGOLI YA LIVER POOL YALIFUNGWA NA
- R. Dunne 67' (own goal),
- Philippe Coutinho 90',
- S. Caulker 90'+ (own goal)
- HUKU MAGOLI YA QPR YAKIFUNGWA NA
- E. Vargas 87', 90'+
0 comments :
Post a Comment