-->

MCHEZAJI MAARUFU AFRIKA APIGWA RISASI NA KUFARIKI DUNIA WALIPOJARIBU KUMFIKISHA HOSPITALI

SENZO-MEYIWANAHODHA wa Timu ya Taifa ya Afrika Kusini, Senzo Meyiwa, ambae ni Kipa, ameuliwa kwa kupigwa risasi.
Habari hizi zimethibitishwa na Polisi wa Afrika Kusini ambao wamesema Kipa huyo wa Bafana Bafana na Klabu ya Orlando Pirates aliuawa nyumbani kwa Gelfrendi wake huko Vosloorus, Kusini mwa Mji wa Johannesburg.
Senzo Meyiwa, aliekuwa na Umri wa Miaka 27, Jumamosi aliidakia Orlando Pirates walipoifunga Ajax Cape Town Bao 4-1 na kutinga Nusu Fainali ya Kombe la Ligi la Afrika Kusini.
Kwenye Taarifa yao, Polisi wamesema Watu wawili waliingia ndani ya Nyumba aliekuwemo Meyiwa na wa Tatu alibakia nje walipokuwa wakijaribu kuiba.
Watu hao Watatu walikimbia baada ya kufyatua risasi.
Polisi wamesema watatoa zawadi ya Dola 14,000 kwa yeyote atakaetoa taarifa za kukamatwa kwa Wahalifu hao.
Meyiwa alianza kuichezea Orlando Pirates Mwaka 2005.
Akionglea msiba huu, Mwenyekiti wa Orlando Pirates, Irvin Khoza amesema: “Huu ni msiba mkubwa kwetu na Familia ya Senzo, Orlando Pirates na Taifa.”
Msimu uliopita Senzo Meyiwa alidaka wakati Orlando Pirates inafungwa Jumla ya Mabao 3-1 na Al Ahly ya Misri katika Mechi mbili za Fainali ya CAF CHAMPIONZ LIGI.
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment