Kuna
mjadala wa muda mrefu kuhusu suala la nyama nyekundu, ambapo makundi
mawili tofauti yamekuwa yakitoleana hoja kuhusu faida na madhara ya kula
nyama, hasa ile nyama iliyowekwa katika kundi la ‘nyama nyekundu’ (red
meat).
Wakati
wakereketwa wa masuala ya afya wanasema kuwa nyama nyekundu huchangia
hatari ya mtu kupata ugonjwa wa moyo na saratani ya tumbo, wadau wa
nyama wanadai kuwa hakuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya saratani,
ugonjwa wa moyo na nyama nyekundu.
Wakereketwa
wa masuala ya afya wanaeleza kuwa ukweli uko wazi kwamba nyama nyekundu
inaweza kusababisha ugonjwa wa moyo kwa mtumiaji, kwani baadhi ya nyama
nyekundu huwa na kiwango kikubwa mafuta (saturated fat) ambayo huongeza
kolestro mwilini na mtu mwenye kiwango kikubwa cha kolestro huwa
hatarini kupatwa na ugonjwa wa moyo.
Kwa
upande wa saratani, watafiti wanasema kuwa bado hakujawa na ushahidi wa
moja kwa moja kuwa nyama nyekundu inaweza kusababisha saratani ya
tumbo. Utafiti wa hivi karibuni uliofanywa na Taasisi ya Afya ya Taifa
nchini Marekani, umebaini kuwa watu wanaopenda kula kwa wingi nyama
nyekundu, hufa mapema kuliko wale wanaokula kiasi kidogo cha nyama hiyo.
Wapenda
nyama ambao wako kwenye hatari kubwa ya kupatwa na saratani na ugonjwa
wa moyo ni wale wanaokula kuanzia kiasi cha gramu 112 za nyama (karibu
robo kilo) kila siku, lakini wanaokula kiwango kidogo (nusu ya robo
kilo) hawako hatarini na badala yake watapata virutubisho muhimu
vinavyopatikana kwenye nyama.
Ulaji
wa nyama nyekundu wenye faida kwa mwili wa binadamu ni ule unaozingatia
kiasi na aina ya nyama. Nyama inayopendekezwa ni steki isiyo na chembe
ya mafuta (lean meat) na itakayoliwa kwa kiasi kidogo.
Nyama
inahitajika kiafya kwasababu ina madini ya chuma ambayo ni muhimu kwa
wasichana na wanawake wanaotarajia kuzaa. Pia nyama ina Vitamini B12
ambayo husaidia utengenezaji wa DNA na hujenga mishipa na seli za damu.
Halikadhalika kuna madini ya zinki ambayo husaidia kuimarisha ufanyaji
kazi wa kinga ya mwili. Bila kusahau nyama ina protini ambayo ni muhimu
kwa ujenzi wa mifupa na misuli
Kwa
ujumla, nyama nyekundu ni muhimu kwa afya ya binadamu, lakini itakuwa
muhimu kama itatumiwa kwa kiwango na kiasi kinachotakiwa. Siku zote
epuka kula nyama yenye mafuta na badala yake pendelea kula steki
isiyokuwa na mafuta ili upate virutubisho vyake muhimu kwa afya yako.
Kula
nyama kinyume na mwongozo huu, ni sawa na kuamua kujiweka katika hatari
ya kupatwa na ugonjwa wa moyo na matatizo mengine ya kiafya, ikiwemo
ugonjwa wa miguu au kansa ya tumbo. Jiepushe na hayo kwa kuzingatia
masharti ya ulaji sahi
0 comments :
Post a Comment