MGAWANYO
wa ruzuku na kikwazo cha Sheria ya Vyama vya Siasa, vinatarajiwa
kugeuka kisu kikali, kitakachotishia muungano wa vyama vinavyounda
Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), vya Chadema, CUF na NCCR-Mageuzi.
Tayari
Ukawa imetangaza nia ya kusimamisha mgombea mmoja katika uchaguzi wa
serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Desemba mwaka huu, na mgombea
udiwani, ubunge na urais mmoja katika uchaguzi mkuu ujao,
utakaofanyika mwakani.
Mwenyekiti
wa Ukawa, Profesa Ibrahim Lipumba, alitoa tamko la mgombea mmoja jana
mbele ya waandishi wa habari, ambapo alifafanua kuwa,
mgombea huyo katika kila nafasi kuanzia kitongoji mpaka urais, atateuliwa kwa kufuata vigezo
vitakavyokubaliwa na vyama hivyo.
Alisema
uchaguzi huo wa serikali za mitaa, kwao ni nguzo muhimu ya kufikia
malengo yao ya kushika dola na hatua hiyo itathibitisha kuwa Ukawa ni
ushirikiano thabiti, ulioazimia kuwapa
wananchi njia bora ya ukombozi.
Katika
kudhihirisha nia hiyo, Profesa Lipumba alisema Oktoba 26 mwaka huu,
wanatarajia kusaini makubaliano ya pamoja ya wanachama wa Ukawa, katika
mkutano wa hadhara utakaofanyika jijini Dar es Salaam.
SHERIA
Hata hivyo, tamko hilo la Profesa Lipumba, halikufafanua changamoto iliyotolewa hivi karibuni
na aliyekuwa Msajili wa Vyama vya Siasa, John Tendwa, kwamba Ukawa hauwezi kuweka
mgombea mmoja katika mazingira ya sasa ya Sheria ya Vyama vya Siasa.
Tendwa
alitaka vyama hivyo kabla ya kufikia hatua hiyo, vipigie kampeni
Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Vyama vya Siasa, ambao aliuacha
ofisini kwake kabla ya kustaafu, kwa kuwa unaruhusu wao kuungana na kuweka mgombea mmoja.
Kwa mujibu wa Tendwa, kwa sheria ya sasa ya vyama hivyo vinaweza kumuunga mkono mgombea wa chama fulani, lakini haviwezi kuwa
na umoja utakaopewa jina, kisha kusimamisha mgombea mmoja huku kila chama kikibaki na utambulisho wake.
Tendwa ambaye alizungumza na gazeti moja la kila siku, kuhusu utata wa kuweka mgombea mmoja, alisisitiza kwamba Ukawa hawawezi
kuutumia kusimamisha mgombea mmoja katika Uchaguzi Mkuu.
Alifafanua
kuwa muungano huo wa Ukawa sio wa kisheria, hauwezi kuweka mgombea
mmoja wa urais na kumuita mgombea wa Ukawa kwa kuwa
sheria haisemi hivyo.
RUZUKU
Mbali
na sheria, Tendwa pia alisema hata utaratibu huo ukianzishwa na vyama
hivyo vikapata nguvu ya kisheria kuungana na hivyo kuweka mgombea mmoja,
ni lazima upatikane
ufumbuzi kuhusu ruzuku. Kwa mujibu wa Tendwa vyama hivyo vitatakiwa
kujiridhisha ruzuku itakwenda wapi, kama ni katika umoja au chama kupitia mbunge.
Alitoa
mfano wa Kenya, ambako Sheria inaruhusu vyama kuungana na kuweka
mgombea mmoja, ambako alisema wanachofanya ni asilimia fulani
ya ruzuku kwenda katika umoja na inayobaki kuingia kwenye chama kupitia mbunge. Upungufu uchaguzi
Pamoja
na kutangaza nia ya kuweka mgombea mmoja katika uchaguzi wa serikali za
mitaa bila kujali mazingira magumu ya kisheria yaliyopo, Profesa
Lipumba pia alisema baada ya kupitia
kanuni za uchaguzi huo, wamebaini upungufu mkubwa ambao wanahitaji kupata ufafanuzi wa kina.
Alitaja
mambo ambayo alisema yana upungufu kuwa ni idadi ya siku za kuandikisha
wapiga kura kutowekwa wazi kwenye kanuni, utata wa fomu za
wagombea na karatasi ya wapiga kura inayohusu wao kutakiwa kujaza nembo ya chama na halmashauri.
Pia
alihoji kwanini muda wa mwisho wa kampeni, umewekwa saa 11 jioni wakati
kwa Sheria ya Vyama va Siasa inaweka wazi kuwa muda wa mikutano ya
siasa ni saa 12 jioni.
Dk Slaa
Kwa
upande wake Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Wilbrod Slaa alisema, kwa sasa
wanajipangabkuhakikisha Katiba Inayopendekezwa inapingwa
kwa nguvu zote, ambapo alisema watahakikisha wanatoa elimu kwa wananchi ili waikatae katiba
hiyo popote walipo.
“Iwe ni vijiweni kwenye kahawa, mashambani, majumbani au kwingine kokote kule. Tutahakikisha haki za Watanzania zinadaiwa kwa
nguvu zote na kile walichokileta wao (Katiba Inayopendekezwa), kinapingwa kwa nguvu zote,” alisema Slaa.
Hata
hivyo,Ukawa watakabiliana na upande mwingine unaotoa elimu ya kuikubali
Katiba hiyo, unaoungwa mkono na asasi za kiraia, Chama Cha
Mapinduzi na hata Rais Jakaya Kikwete.
Kwa
mfano, Rais Kikwete alipokuwa ziaranibMwanza hivi karibuni alisema;
“Sijui Katiba nyingine duniani ambayo inajadili makundi yote ndani ya
jamii kama hii Katiba Inayopendekezwa.
“Hakuna
aliyeachwa – wavuvi wamo, wajane wamo, wafanyabiashara ndogo wamo,
akinamama lishe wamo, wakulima wamo, wafugaji wamo….kila
mtu yumo.
"Akinamama ndio usiseme kabisa wao wamepata hata asimilia 50 kwa 50 ndani ya Bunge." Aliongeza Rais Kikwete:
“ Hivi Katiba mbaya inakuwa kama
inayopendekezwa na kama hii inayopendekezwa ni mbaya sasa hivi nzuri ikoje?”
SOURCE:AFRICAN NEWS
0 comments :
Post a Comment