Mabaki ya mwili yaliyokutwa katika eneo la kijiji cha Lupapila wilaya ya songea mkoaniRuvuma yakikusanywa na wataaramu kutoka hospital ya mkoa wa Ruvuma.
Fuvu la kichwa likiwa linazolewa
-------------
Na Amon Mtega wa Demasho.com Songea
MIFUPA ya masalia ya binadamu wa jinsia ya kiume ambaye hakuweza
kufahamika jina na kukadiliwa kuwa na miaka (30) yamegundulika na
Zaujia Pilly (70) mkazi wa kijiji cha Lupapila wilaya ya songea mkoani
Ruvuma wakati akienda kuchimba dawa za kienyeji baada ya kuwaona mbwa
wakishambulia sehemu za mabaki hayo.
Akiongea na MTANDAO HUU ofisini kwake jana Kamanda wa polisi mkoa wa
Ruvuma Mihayo Msikhela alisema kuwa tukio hilo limetokea oktoba 26
mwaka huu majira ya saa 9:45 alasiri huko katika kijiji cha Lupapila
mtaa wa Mahinya kata ya Subira nje kidogo ya manispaa ya Songea.
Alisema kuwa inadaiwa siku hiyo ya tukio kwenye msitu wa uwanja wa
ndege ilikutwa mifupa ya binadamu wa jinsia ya kiume ikiwemo fuvu la
Kichwa, Mbavu, Mikono na Miguu wakati sehemu ya kiuno na mapaja ikiwa
imeharibika vibaya.
Alifafanua kuwa mabaki ya mwili huo yaligunduliwa na Zaujia Pilly
wakati akienda kuchimba dawa za kienyeji kwenye msitu huo ghafla
aliwaona Mbwa wakifukuzana kugombania mabaki ya mwili wa binadamu.
Alieleza zaidi kuwa Zaujia baada ya kugundua tukio hilo alitoa
taarifa katika uongozi wa serikali ya Mtaa na kisha taarifa
zilipelekwa katika kituo kikuu cha polisi cha songea mjini ambako
baadaye polisi walifika eneo la tukio wakiwa wameongozana na Daktari
kutoka hospitgali ya Mkoa wa Ruvuma ambaye aliyafanyia uchunguzi
mabaki ya mwili huo na kubaini kuwa marehemu alikuwa amepigwa na kitu
kizito kichwani kwenye eneo la kisogo kilichopelekea kifo chake.
Kamanda Msikhela alisema kuwa kufuatia tukio hilo hakuna mtu yeyote
anayehusishwa na jeshi la polisi mkoani Ruvuma linaendelea kufanya
uchunguzi wa kina juu ya kifo hicho.
CDT: Demasho.com
0 comments :
Post a Comment