-->

DONDOO ZA AFYA:HIZI NDIO NJIA NYEPESI ZA KUPAMBANA NA MBU,SOMA HII NI MUHIMU SANA

Njia hizi mbali mbali wanatumia wenzetu kupunguza mbu majumbani kwao.

1.Beseni la alkali.

Beseni hilo baada ya kumwaga maji, chini ni mayai ya mbu yaliyokufa.

Weka sabuni ya kufulia ya unga na vipande vya sabuni ya kufulia ya mche kwenye beseni dogo lenye maji, kisha weka chini ya kitanda au sehemu yoyote yenye giza iliyojificha.Baada ya siku tatu utakuta mbu wamepungua nyumbani kwako.
Sababu: Harufu ya maji ya sabuni itawavutia mbu kutaga mayai kwenye maji hayo, lakini mayai hayataweza kuishi humo kutokana na alkani ya sabuni.Kutokana na kuwa mbu hao hawataweza kuzaliana na ufupi wa maisha ya mbu, basi mbu watapungua au kuisha kabisa kama hakutakuwa na mbu watakaoingia toka nje.

2.Ushawahi kukaa na wenzako, ukakuta mbu wanakung'ata wewe peke yako tuu? wenzako hata hawalalamiki, basi damu yako tamu sana, jaribu kula vitu vitakavyofanya damu yako iwe chungu kama ya wenzako pia. Kuna harufu ambazo mbu wanachukia, harufu ya vitamin B1, kama una mkesha wa nje, siku tatu au nne kabla kula vyakula vyenye vitamin B1 kwa wingi, baada ya hapo hata usipojifunika mbu watakimbia wenyewe.Ama kama una vidonge vya vitamin B1, pia unaweza kuvidilute kwenye maji na kisha kujipanga kwa ngozi, mbu watakimbia wenyewe bila hata ya wewe kukohoa.

3.Tumia star anise na shamari(fennel) mbili kwa kila moja, weka kwenye beseni au maji ya kuoga kisha oga, mbu hawatakusumbua kabisa.
shamari

shamari

star anise

star anise

 4.Unguza ganda la chungwa ndani ya chumba au sebule, hii itafukuza mbu, na pia itafanya nyumba yako inukie vizuri.

5.Badilisha mara kwa mara maji ya maua/mimea uliyoweka sebuleni au chumbani.

6.Usitumie dawa ya aina moja ya kuua mbu, ni vizuri kama unatumia dawa kubadilisha aina/brand kila baada ya miezi miwili.

7.Kula vitunguu kwa wingi, mbu hawapendi harufu inayotoka kwenye mwili wa mtu alikula vitunguu.

8.Kipindi cha usiku weka maua ya jasmini, milani au ua waridi pale ambapo hutaki mbu wasogee, mbu hawapendi harufu za maua hayo hivyo hutoka nduki punde tu wanaposikia harufu hizo.

9. Kama ukiweza weka taa za rangi ya orange/chungwa, mbu wanaogopa rangi ya chungwa hivyo ukiweka taa za rangi hiyo basi hawatasogea, na waliopo watatoka baruti.

10.Majani ya chai yakiunguzwa, moshi wake pia unaweza kufukuza mbu na wadudu wengine.

Kusoma ni busara, kugawana na wenzako ni wema, makala nzuri si vyema kujisomea peke yako, ni bora kugawana na wenzako, tembeza ujumbe mzuri kwa wenzako pia wafaidike, unaweza kushare kwa facebook, google+ na kadhalika!
SOURCE:JICHO LA UCHINA
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment