Matokeo ya awali ya uchaguzi nchini Msumbiji yanaonesha Filipe Nyusi kutoka chama tawala cha Frelimo ameshinda urais.
Nyusi amepata asilimia 57 ya kura, huku Afonso Dhlakama kutoka chama kikuu cha upinzani cha Renamo akipata asilimia 36.
Frelimo pia imeendelea kushikilia viti vingi bungeni, 250, lakini chama hicho kimepoteza viti 49 ukilinganisha na mwaka 2009.
Chama cha Renamo kimepinga matokeo hayo, kikisema kulikuwa na ukiukwaji mkubwa wa utaratibu wa uchaguzi.
SOURCE:SALIM KIKEKE
0 comments :
Post a Comment