Cristiano
Ronaldo amekomba zawadi tatu 'hat trick' za tuzo ya wachezaji bora Ligi ya Hispania maarufu
kama La Liga.
Huku mpinzani wake Lionel Messi akiambulia patupu, tuzo
tatu alizobeba Ronaldo ni pamoja na Mchezaji Bora, Mfungaji Bora na
Mshambuliaji Bora wa La Liga.
Ilikuwa
furaha kubwa kwa Ronaldo ambaye aliongozana na mpenzi wake Iryna Shayk,
mwanamitindo kutoka Urusi.
Pamoja
na Ronaldo kubeba tuzo hizo, timu yake ya Real Madrid imetawala zaidi kuliko
klabu nyingine ya Hispania.
Zawadi
ya kiungo bora imekwenda kwa Luka Modric huku Sergio Ramos akichukua tuzo ya beki bora.
Kipa
mpya wa Real Madrid, Keylor Navas amechukua tuzo ya mlinda mlango bora. Kabla ya
kutua Madrid, Navas alikuwa akikipiga Levante.
Barcelona
pia imefanikiwa kupata tuzo tatu, Andrés Iniesta alitangazwa kuwa kiungo bora
mshambuliaji, huku Ivan Rakitic na Rafinha wakitwaa tuzo mbili za Fair Play and
Breakthrough.
Kutokana
na mafanikio makubwa msimu uliopita, Kocha wa Atlético, Diego Simeone alibeba
tuzo ya Kocha Bora.
Mshambuliaji nyota wa Sevilla, Carlos Bacca akachukua tuzo mchezaji Bora kutoka Amerika Kusini na Yacine Brahimi wa Granada akawa Mchezaji Bora kutoka Afrika.
0 comments :
Post a Comment