-->

DONDOO ZA AFYA:UFAHAMU UGONJWA WA MABUSHA NA DALILI ZAKE

Mabusha ni hali ya kujaa maji kwenye mfuko wa pumbu. Hali hii hutokea kunapokuwa na
mkusanyiko wa maji kati ya tabaka mbili za utando unaozunguka korodani. Kwa hapa nchini,
tatizo hili ni maarufu sana maeneo ya mwambao wa Pwani ya Bahari ya Hindi, kiasi cha kuhusishwa na imani kadhaa kama unywaji wa maji ya madafu. Aidha, tatizo hili limekuwa likichukuliwa na baadhi ya watu kuwa ni hali ya kudhalilisha ingawa kwa wengine huonekana ni hali ya kuwa ‘mzee wa heshima’ au ‘umwinyi’.


Ifahamike pia kuwa, tatizo la mabusha halitokei kwa wanaume watu wazima tu. Watoto wa kiume hususani katika mwaka wa kwanza (infants) pia ni waathirika wakuu wa tatizo hili.
Kwa kawaida mabusha hayana maumivu na wala hayaleti madhara, isipokuwa kama
yatapata uambukizi kwa sababu nyingine yeyote ile, hali inayowafanya wengi wa waathirika, hasa wa mwambao, kuwa wagumu kutafuta ufumbuzi wa tiba. Hata hivyo, ni vyema kama mtu ana uvimbe wowote kwenye pumbu zake, kutafuta msaada wa kitabibu ili kuweza kuondoa
uwezekano wa kuwepo kwa magonjwa mengine ya sehemu za siri kama vile saratani ya
korodani (testicular cancer) n.k. 

Mabusha husababishwa na nini?
Sababu za kutokea kwa mabusha hutofautiana kati ya watoto wa kiume na wanaume watu wazima.
Kwa watoto wa kiume  mabusha huweza kuanza kutokea kipindi wako tumboni wakati wa ujauzito, korodani za mtoto wa kiume huwa kwenye tumbo lake kabla ya kushuka taratibu kuelekea kwenye
mapumbu. Wakati wa ushukaji huo, kifuko kinachozunguka korodani kinachoitwa processus vaginalis hushuka sambamba na kurodani hizo na
kufanya korodani kuzungukwa na maji. Kwa kawaida, ndani ya muda wa mwaka mmoja, kifuko hiki
hufunga na maji hayo yanayozunguka korodani yote hufyonzwa na kurudishwa kwenye tumbo la mtoto. Iwapo baada ya kifuko kufunga na maji yaliyomo kushindwa kufyonzwa kurudishwa kwenye
tumbo la mtoto, mtoto hupata busha lijulikanalo kitaalamu kama busha lisilo na
mawasiliano (non-communicating hydrocele). Hali kadhalika, wakati mwingine inawezekana kifuko
kikashindwa kufunga na hivyo maji yakaendelea kujaa ndani ya kifuko kuzunguka korodani.
Aina hii ya mabusha kwa watoto ujulikana kama busha lenye mawasiliano
(communicating hydrocele).

Kwa wanaume watu wazima Kwa wanaume watu wazima, mabusha husababishwa na
mambo makuu mawili;

1.Kwanza, kitendo chochote kinachochochea tando zinazozunguka korodani kuzalisha maji kwa wingi kuliko kawaida,
2. pili ni kupungua kwa ufyonzaji wa maji yanayozunguka korodani kwa sababu ya kuziba kwa mirija ya lymph (blockage of scrotal lymphatic system) au kuziba kwa mishipa ya damu
inayosafirisha damu kutoka kwenye pumbu kwenda sehemu nyingine za mwili (blockage of scrotal venous system).

3. Ongezeko la uzalishaji wa maji linaweza kutokana na
Maambukizi au/na majeraha katika korodani (testicular
inflammation au orchitis) au maambukizi katika mshipa ujulikanao kama epididymis yanayoweza
kusababishwa na kifua kikuu (tuberculosis) cha
makende, au maambukizi yanayosababishwa na vimelea wa filaria (filariasis) wanaosababishwa
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment