Mamia ya Waislamu wa mji wa Quimper kaskazini magharibi mwa Ufaransa wamefanya maandamano wakiitaka serikali ya nchi hiyo iruhusu ujenzi wa msikiti katika mji huo.
Maandamano hayo yaliyofanyika katika moja ya medani za katikati ya mji huo, yamelaani kusuasua kwa serikali na kutoruhusu ujenzi wa msikiti huo.
Mkuu wa kituo cha haki za wahamiaji katika mji huo wa Quimper, Marie-Madeleine Le Bihan amewambia waandishi wa habari kwamba maandamano hayo yanafanyika kupinga ubaguzi, ufashisti, na kukosekana usawa dhidi ya jamii ya Waislamu.
Marie ameongeza kuwa, raia wote wa Ufaransa wana haki sawa ya kufanya ibada zao za kidini na kimadhehebu kwa uhuru.
Ufaransa ni miongoni mwa nchi za Ulaya zinazoongoza kwa ubaguzi wa kidini dhidi ya Waislamu. Ripoti zinaonyesha kwamba vitendo vya ubaguzi dhidi ya dini ya Uislamu na Waislamu kwa ujumla vimeongezeka zaidi nchini humo.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo vitendo hivyo viliongezeka na kukaribia asilimia 50 katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita huku matukio ya ubaguzi dhidi ya Waislamu yakizidi kushika kasi siku hadi siku nchini humo.

0 comments :
Post a Comment