-->

STAZI WAWACHINJA WAMOROCCO BAO 3-1

          Thomas Ulimwengu akimtoka beki wa MOROCCO kwenye mchezo dhidi ya STAZ
Timu ya taifa ya TANZANIA ambayo ni maarufu kama TAIFA STARS hapo jana walifanikiwa kumtandika MOROCCO bao tatu kwa moja(3-1) na kuwafanya Watanzania kuisogelea nafasi ya pili wakiwa nyuma ya Ivory coast kwa pointi moja kwani yenyewe ina pointi 7 na Taifa Stars ina pointi 6,
magoli ya Taifa Stars yaliwekwa kinywani na wachezaji wawili wanaocheeza soka la kulipwa nchini Congo katika klabu ya TP Mazembe,Thomas Ulimwengu na Mbwana Samata.Goli la kwanza lilifungwa na Ulimwengu katika dakika ya 45 kisha goli la pili lilifungwa na Samata katika dakika ya 67 baada ya kuwazidi mbio mabeki wa Morocco kwa kuuchukua mpira pigwa kutoka katikati ya uwanja na kuutia nyavuni.Samata hakuhishia hapo bali aliendelea kuwanyanyua mashabiki kwa kutandika bao la 3 katika dakika ya 78 kwenda 79 bao ambalo lilipelekea kutoka kwa kadi nyekundu kwa mchezaji wa Morocco aitwae Barrad Abdelaziz kwenye dakika ya 80 kwa kumtolea maneno machafu muamuzi.Katika dakika za lala salama Morocco iliambulia kupata bao la kufutia kwenye dakika ya 90 baada ya kuongezwa dakika 3.
Mpaka mpira unaisha TAIFA STAZ 3-1 MOROCO
Nahuu ndio msimamo wa kundi hili la TANZANIA kwa sasa
KUNDI C
1 Côte d'Ivoire Mechi 3 Pointi 7
2 Tanzania Mechi 3 Pointi 6
3 Morocco Mechi 3 Pointi 2
4 Gambia Mechi 3 Pointi 1
Endapo kama TAIFA STAZ itapita kwenye kundi hili ambalo anahitajika mshindi mmoja tu atapata nafasi ya kucheza roundi ya tatu ambayo itategeme droo lizunguushwe ili ifahamike nani atacheza na nani.Hapo itakuwa ni mechi mbili tu ambayo ni nyumbani na ugenini na mtu atakaeshinda basi ndie amefuzu kwenda BRAZIL kwa ajili ya kombe la dunia 2014 
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

2 comments :

  1. mungu ibariki Taifa starz mungu ibariki Tanzania, tumeshachoka kuwa vinchwa vya wandazimu kila siku!!!!!

    ReplyDelete
  2. IBARIKI TAIFA STARS ILI ISONGE KOMBE LA DUNIA

    ReplyDelete