-->

MHESHIWA RAISI JAKAYA MRISHO KIKWETE ATIMIZA ZOEZI LA KUZINDUA JENGO LA ICT NA SAYANSI

Baada ya siku hi ya tarehe 14 kusubiliwa kwa hamu na viongozi pamoja na wanafunzi wa chuo kikuu cha kiislam(Muslim University of Morogoro) kwa hamu hatimae leo zoezi hilo limefanikiwa kwani mheshimiwa Raisi Jakaya Mrisho Kikwete alifanikiwa kufika katika Chuo kikuu cha Waislam Morogorona  kufanikisha uzinduzi wa majengo mawili yaliyofunguliwa rasmi na Raisi huyo wa awamu ya nne Mheshimiwa Raisi Dk Jakaya Mrisho Kikwete.
Picha ya hapo juu inamuonyesha Hajjat Mwantumu Malale ambe ndio Mkuu wa chuo kikuu cha waislam Morogoro akiwa na mgeni ambae ni Raisi wa nchi hii ya Tanzania Mheshiwa Raisi Jakaya Kikwete akizindua rasmi jengo la ICT(jengo la teknolojia ya habari).
Picha ya hapo inamuonyesha Makam mkuu wa chuo Professor Mustapha Njozi akitoa maelekezo kwa mgeni rasmi Mheshiwa Raisi Jakaya Mrisho Kikwete kuhusu mradi wa ujenzi wa jengo la teknolojia ya habari.mbele yao ni ubao wenye mchoro wa jengo hilo jinsi litakavyokuwa pindi litakapokamilik.
Picha ya hapo juu inamuomyesha Mheshimiwa Raisi Jakaya Mrisho Kikwete akifungua pazia ili kukamiliza uzinduzi wa jengo la sayansi.Jengo hilo limejengwa chini ya udhamini wa ISLMIC FOUNDATION na anayeonekana na kanzu ni mwenyekiti wa taasis hiyo ya ISLAMIC FOUNDATION Shekh Alif Nahd.


Picha ya hapo juu inamuonyesha Professor Juma Mikidadi aiwa amekaa karibu na mkuu wa chuo Hajjat Mwantumu Malale,akiwa amefuatiwa na Mheshimiwa  Jakaya Mrisho Kikwete na mwisho kabisa ni Makamu mkuu wa chuo Professor Mustapha Njozi wakiwa wanajianda kupiga picha ya pamoja na mheshiwa Raisi kwa ajili ya kumbukumbu.
Sherehe hii ya uzinduzi imefanyika leo tarehe 14/03/2013
picha na Mussa Saidi Mussa
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment