-->

BABA AMUUA MWANAE NA KUMFUKIA SEBULENI KWAKE


Tarehe 27 mwezi wa tatu huko mkoani mbeya katiaka kitongoji kinachoitwa Iponjola,kijiji cha Isange wilaya ya Rungwe ilifahamika siri ambayo ilidumu kwa muda kidogo ya kwamba mtu mmoja anayefahamika kwa jina la Riziki Saidi Mwangoka ambaye ni baba wa mtoto anayefahamika kwa jina la Debora Riziki alimuawa mtoto wake mwenyewe wa kumzaa kwa kumuua na kumfukia katika nyumba yake,Hivyo mtoto huyo alipoteza uhai kwa kuuawa na baba yake mzazi.Bwana huyo alikuwa na ugomvi wa kindoa na mkewe bi Esther Msafiri Mwambenja hivyo kupelekea kutengana kwao na baadae likaibuka swala la nani alee mtoto na ndipo siku moja bwana huyo Riziki alikwenda kumchukua mtoto wake na kwenda kumfukia chumbani kwake tarehe 28/11/2011 na hapo taehe 27/3/2013 ndipo ilipofahamika siri hiyo iliyovujishwa na yeye mwenye.Mtuhumiwa amekwisha kamatwa na harakati za kupelekwa mahakani zinaendelea na mwili wa marehemu Debora Riziki ulifanyiwa uchunguzi na kurejeshwa kwa wanandugu kwa mazishi.
Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya kamishna msaidizi Diwani Athumani aetoa ushauri kwa wanandoa kwamba wasichukue maamuzi mkononi bali wanapaswa kukaa mezani na kuyajadili maswala yao ya ndoa.
Blog hii inakemea vkali vitendo vya kiuwaji kama hivi na vinavyofanana na hivi
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment