-->

GESI ITAKAYOSAFIRISHWA KWRENDA DAR NI ASILIMIA CHACHE TU YA GESI YOTE


Mheshimiwa raisi Jakaya Mrisho Kikwete ametoa kauli yake kuhusu swala la gesi ya Mtwara kwamba si Gesi yote ambayo itachukuliwa kupelekwa Dar es salaam...pia amesema hawezi kuutupa mkono mkoa wa Mtwara wala mkoa wowote ule wa kusini kama alivyonukuliwa katika akaunti yake ya twitter
 "Gesi itakayoletwa Dar es Salaam ni 16% ya gesi yote iliyoko Mtwara kwa miaka 20 ijayo. 84% ya gesi itabaki Mtwara kwa ajili ya kuuzwa nje."Pia alinukuliwa akisema
"Tunawathamini wananchi wa Mtwara. Nitakuwa mtu wa mwisho kuwatupa mkono na kuwapuuza wananchi wa Kusini na sitaruhusu mkoa wowote kupuuzwa"
Ama katika tweet nyingine Mheshimiwa raisi Jakaya Kikwete ametoa shukrani za dhati kwa viongozi wa dini ambao wameshiriki katika namna moja au nyingine katika kutoa ufafanuzi wa swala hilo la gesi
" Shukrani za dhati kwa viongozi wa dini, wazee wa Mtwara, wanasiasa & taasisi mbalimbali zilizojikita katika kuelewesha wananchi juu ya haya."Pia aliongezea kuwa
"Ujenzi wa kiwanda cha saruji na kile cha mbolea (Dangote) bado unabaki kusini na hakujawahi kuwa na mpango wowote wa kuhamisha jambo hilo.
hayo yalikuwa maneno ya Mheshiwa Raisi Jakaya Mrisho Kikwete .
source: https://twitter.com/jmkikwete
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment