RIO
Ferdinand, Nemanja Vidic na Patrice Evra wamekalia kuti kavu Manchester
United wakati David Moyes akinoa panga tayari kufyeka wachezaji wanane
katika harakati za kujenga kikosi imara.
United
imekuwa katika majanga baada ya kupoteza mechi ya tatu mfululizo ndani
ya wiki moja nyumbani kwa Sunderland Jumanne usiku, na Moyes anataka
kuwapiga chini wachezaji kadhaa wasiotakiwa na waliokosa furaha ili
kurejesha heshima ya klabu.
Nyota
hao watatu wa safu ya ulinzi wanatarajiwa kuungana na Javier Hernandez
‘Chicharito’, Nani, Anderson, Alex Buttner na Anders Lindegaard.
Kama
kweli Moyes atatimiza mpango huo na kuwatupia virago Ferdinand, Vidic
na Evra, ni wazi atapoteza uzoefu wa zaidi ya mechi 1,000 ndani ya
United na mataji makubwa 30.
Ferdinand
(35) amecheza mechi 444 na kufunga mabao 8 akiwa na jezi ya United,
huku msimu huu akicheza mara 13; akiwa amebeba mataji 10 makubwa
(Premier League (6), Champions League, League Cup (2), World Club Cup).
Vidic
(32) amecheza mechi 283, amefunga mabao 19 (msimu huu mechi 19, bao 1)
huku akibeba mataji 10 makubwa (Premier League (5), Champions League,
League Cup (3), World Club Cup).
Evra
(32) amecheza mechi 349, amefunga mabao 9 (msimu huu mechi 31, mabao
2), huku akibeba mataji 10 makubwa (Premier League (5), Champions
League, League Cup (3), World Club Cup).
Wakati
akielezwa kutaka kufyeka nyota hao, bado kuna hatihati kuhusu Wayne
Rooney ambaye bado amegoma kusaini nyongeza ya mkataba mpya huku Robin
van Persie akiwa kwenye kiwango duni tangu kutua kwa Moyes.
United ipo katika mwendo mbaya zaidi unaochagizwa na kiwango kibovu – rekodi ambayo kwa mara ya mwisho iliwakumba mwaka 1992.
0 comments :
Post a Comment