Naibu
katibu Mkuu wa CCM-Bara Mh:Mwigulu Nchemba akiwasili eneo la Mkutano wa
hadhara Kata ya PARTIMBO kitongoji cha NALANG,TOMON Wilaya ya Kiteto
hii leo tar.25.01.2014 kwaajili ya Ufunguzi wa Kampeni za Uchaguzi mdogo
wa Udiwani kata ya Partimbo.Kata hii miaka yote imekuwa Ikiongozwa na
CCM hadi Mauti yalipomkuta Diwani mwaka jana 2013.Vyama vya Siasa
vilivyosimamisha wagombea wake kwenye kata hii ni CCM(Watetezi wa
Kiti),CHADEMA na TLP.
Naibu
Katibu Mkuu CCM akiwapungia Mkono mamia ya Wananchi waliojitokeza
kwenye Mkutano wa Ufunguzi wa Kampeni za Udiwani Kata ya partimbo.
Mh:Mwigulu
Nchemba akizungmza na Wananchi waliojitokeza kwa wingi kwenye Ufunguzi
wa Kampeni hapa Kiteto,Sehemu kubwa ya Wananchi wanaoishi hapa ni
Wakulima na Wafugaji.Mh:Mwigulu Nchemba amewaomba Wanapartimbo kumchagua
Mgombea wa CCM kwa sababu ndio wanaounda Serikali na ndicho chama
chenye Ilani inayotekelezwa ndani ya Kata hiyo.Pia Mwigulu ameowaomba
Wananchi wa Partimbo kupuuzi watu wanaopitapita mitaani na kuchochea
Vurugu za Wakulima na Wafugaji kwa maslahi yao ya Kisiasa."Nawaomba sana
umoja wenu uendelee kudumishwa,mmekuwa mkishirikiana kwenye kazi nyingi
hapa kati ya Wakulima na Wafugai,Vurugu zozote zile kati yenu ni
manufaa kwa Vyama fulani ambavyo vinaishi kwa kutegema Uvunjifu wa Amani
na kumwaga damu za Watanzania wasio na Hatia.
Alisisitiza,CCM
imekuwa balozi wa Amani nchi hii kuanzia Uhuru,lakini Mfumo wa Vyama
Vingi umeleta vyama vinavyokuwa Mabalozi wa Uvunjfu wa Amani,Hivyo
ndivyo vinavyozunguka ndani ya Nyumba zenu na Kuwagawa kwa Misingi ya
Ukulima wenu na Ufugaji wenu.Hawana nia nzuri dhidi yenu,Chaguo sahihi
ni CCM kwa maendeleo yenu wenyewe,Nauliza hivi hao wengine mnazijua sera
na Ilani zao?Kwa manaofuatilia vyombo vya habari Ilani ya Chama
kimojawapo ni Kupambana wao kwa wao ilimradi unataka uongozi ndani ya
chama chao,Hii leo wanatumia Mabilioni ya shilingi kupambana na Mtu
mmoja ambaye hana kosa,Wanapambana kutetea kitegauchumi chao,Hivyo
naomba msidaganyike na hao watu,Wao wananufaika na Vurugu zozote
zitakazotokea juu yenu kama walivyonufaika na Vifo walivyovisababisha
kwenye mikutano yao.
Naibu
Katibu Mkuu amkimnadi mgombea wa Chama Cha Mapinduzi kata ya Partimbo
Ndugu Sekemi Maitey Sakana.Jambo la kufurahisha na kuonesha Umoja
uliokomaa miongozi mwa WanaCCM waliokuwa Wagombea kwenye kura za maoni
na Kushindwa,Hii leo wamepanda jukwaani na kuwaomba wananchi wote wa
Partimbo kumuunga mkono Mgombea wa CCM kwasababu ndiye wanaweza kukaa
naye na kumshauri mambo ya kutekeleza kwaajili ya kata yao.Kubwa likiwa
Ujenzi wa Zahanati na Barabara kwaajili ya shuguli za Kiuchumi.
Mh:Mwigulu Nchemba akiteta jambo na Mgombea Udiwani wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Sekemi Sakana.
"Ilani
inayotekelezwa niya CCM,Rais wa CCM,Mbunge ni Wa CCM na Diwani pia
tunahitaji wa CCM.Kiteto kuna Madiwani 26 wa CCM na 3 waupinzani,Sasa
hao watatu wamewasaidia nini kama sio Kuhujumu mipango ya
maendeleo?,Mchagueni Mgombea wa CCM kwasababu ndiye atakaye kuwa
msimamizi wa utekelezaji wa Ilani ya CCM ndani ya kata hii".
Naibu
Katibu Mkuu CCM Bara Mh:Mwigulu Nchemba akiagana na Wananchi wa Kata ya
Partimbo Kitongoji cha Nalang'tomon.Mkutano Ulikuwa Mkubwa tofauti na
Matarajio ya Wakazi wa hapa kutokana na Jamii ya hapa kuwa Wakulima na
Wafugaji hivyo Muda mwingi wanakuwa Machungoni na Wakulima wanakuwa
Mashambani.Lakini Kwasababu ya Maendeleo yao wameamua Kusikiliza Sera za
CCM na Wameahidi Ushindi wa Kishindo kwa Mgombea wa CCM Ndugu,Sekemi
Sakana.
0 comments :
Post a Comment