Inri Cristo, 66, akiongea na wanafunzi (wafuasi) wake nje ya kanisa lake liliopo Brasilia nchini Brazil.
Inri Cristo akiwa katika baiskeli yake nje ya eneo lake la kanisa
Mwana wa mungu
Inri - neno la kilatino ambalo maana yake ni 'Yesu wa Nazareti',
'Mfalme wa wayahudi' ana amini kwamba mahali kanisa lake lilipo ndo
Yerusalemi Mpya'.
Hawa ni
baadhi ya wanafuzi wa Inri Cristo ambao huishi hapo hapo kwenye eneo la
kanisa. Wengi wa wawashiriki hao wamekuwa wakijulikana na Inri kwa zaidi
ya miaka 20.
Pamoja na kwamba ni nyumba ya Yesu na makao makuu ya dehebu la Inri lakini bado hutumia mbwa kwa aajili ya kumlinda.
Wafuasi wa
Inri Christo ambao ni wanawake huvaa nguo za blue ambazo zina logo ya
kanisa hilo, zenye kamba kiunoni na kofia za kufumwa.
Inri Cristo huwahubiria waumini wake kila Jumamosi asubuhi kutoka mimbara yake kwenye mji wake 'Mpya wa Yerusalem'
Inri Cristo
amekuwa akihubiri kama 'Yesu' tangia mwaka 1979. Pichani ni Inri akiwa
amezungukwa na wafuasi wake mwaka 1982 huko Belem Cathedral, Lisbon
nchini Portugal.
Vitu vya Inri hufungiwa kwenye kabati la kioo kwenye kanisa lake huuko Brasilia.
Inri Cristo
akiwa kwenye picha mwaka 1993 huku amevalia taji la miba akitaka
kuwahakikisha watu kwamba yeye ndo Yesu Kristo aliyefufuka.
Mahubiri ya
Inri yamekuwa na utata mkubwa na kumuona akiingia katika matatizo na
sheria hadi kutiwa ndani zaidi ya mara 40 huku nchi zingine zikimwekea
pingamizi kuingia katika nchi zao.
Wanafuzi wa Inri ambao ni wanawake wakimsukuma mimbara yake kuelekea kwenye bustani ili wakasikilize mahubiri yake.
Kweli duniani
kuna vituko vingi sana na huyu Mungu anatafutwa kwa njia zote. Lakini
ndugu zangu tukumbukeni maneno kutoka kwenye kitabu kitakatifu 'BIBILIA'
Matthew 7:15-23 ya kwamba siku za mwisho kutakuwa na manabii wengi
wauongo.
"Jihadharini
na manabii wa uongo. Wao huja kwenu wakionekana kama kondoo kwa nje,
lakini kwa ndani ni mbwa mwitu wakali. Mtawatambua kwa matendo yao. Je,
watu huchuma zabibu katika miti ya miiba, au tini katika mbigili?
La! Basi, mti mwema huzaa matunda mema, na mti mbaya huzaa matunda
mabaya. Mti mwema hauwezi kuzaa matunda mabaya, wala mti mbaya hauwezi
kuzaa matunda mema. Kila mti usiozaa matunda mema utakatwa na kutupwa
motoni. Kwa hiyo, mtawatambua kwa matendo yao.
"Si kila
aniambiaye, `Bwana, Bwana,` ataingia katika Ufalme wa mbinguni; ila ni
yule tu anayetimiza mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni. Wengi
wataniambia Siku ile ya hukumu: `Bwana, Bwana! kwa jina lako tulitangaza
ujumbe wako, na kwa jina lako tuliwatoa pepo na kufanya miujiza mingi.`
Hapo nitawaambia: `Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni mbele yangu, enyi watenda maovu."
CHANZO:BLOGU YA WANANCHI
BOFYA HAPA CHINI KUIPENDEKEZA BLOG YA BUSTANI YA HABARI KWENYE TUZO ZA WEBLOG AWARD 2O14
BOFYA HAPA CHINI KUIPENDEKEZA BLOG YA BUSTANI YA HABARI KWENYE TUZO ZA WEBLOG AWARD 2O14
WEBLOG AWARDS 2014
Original from: http://googlehabari.blogspot.com/2014/01/bustani-ya-habari-inakuomba-wewe-mdau.html
Copyright EXEIdeas - All Rights Reserved
Original from: http://googlehabari.blogspot.com/2014/01/bustani-ya-habari-inakuomba-wewe-mdau.html
Copyright EXEIdeas - All Rights Reserved
0 comments :
Post a Comment