-->

POLISI WAMUOKOA MWANAMKE ALIYETEMBEA NUSU UCHI MITAA YA KARIAKOO


Askari Polisi wa kituo cha Msimbazi Kariakoo Jijini Dar es salaam,wamelazimika kuingilia kati ili kumuokoa mama mmoja asihukumiwe vibaya na vijana wenye hasira.

Tukio hilo la aibu na kufedhehesha limetokea muda huu baada ya mama huyo (asiyejulikana) kupita Kariakoo akiwa katika vazi lenye kuonesha maungo yake na rangi ya mwili wake bila kificho.

Mwanamke huyo mwenye umri kati ya miaka 30 hadi 35 na tano akiwa kavalia taiti nyepesi na laini yenye rangi nyeusi alijikuta anazongwa na vijana wakiopiga miruzi na mayowe na kumfanya ashindwe kuendelea na safari yake.

Kamera ya munira blog ilishuhudia tukio hilo (na kulazimika kupiga picha kwa tahadhari kwa minajili ya kuchunga maadili),ilishuhudia mama huyo akikimbila duka la El Shaddai lililopo mtaa wa Sikukukuu.

Vijana mchanganyiko wakionekana na uchu na hasira walilizonga duka hilo takribani kwa dakika 40 huku wakimshinikiza mwenye duka amfungulie ili wamuadhibu.

"Mtoe huyo,yeye si kaamua kutembea nusu.... basi mlete tumvuwe nguo zote na kisha..... walisikika vijana wakisema kwa hasira"

"kwa kuwa serikali haichukuwi hatua za makusudi ndiyo maana hawa wanatusumbua,sasa ngoja tuisaidie Serikali,wewe msomali mtoe huyo,kama hutaki basi...."kundi jengine lilisikika huku wakipiga miruzi.

Saa 9;42 polisi walifika wakiwa katika gari aina ya toyota na kuanza kuwa tawanya vijana kazi ambayo ilidumu kwa dakika sita na baadae chini ya uongozi wa Afande (aliyejulikana kwa jina la Afande nyoka) askari wakaingia katika duka na kumtoa hali ambayo iliwafanya vijana kuzidi kupiga mayowe wakitaka wakabidhiwe ili wamuadabishe.

"Nashindwa kuelewa ana dhamira gani,kwanza katokaje nyumbani kwake na vazi kama hili,hivyo pale amevaa kweli?Laa haulaa,kwa kweli wanatudhalilisha mno",alisema kwa uchungu mwanamama mmoja aliyevaa vazi la stara.

Saa kumi 9;57 gari la polisi likaondoka kwa kasi na kuwaacha baadhi ya vijana wakilirushia mawe.

Haikuweza kufahamika mara moja nini kinachofuata baada ya kumfiksha polisi msimbazi

chanzo:munira blog
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment