Wazazi wa wanafunzi wa shule zilizoko kusini mwa India katika maeneo ya Kerala wamepinga uamuzi wa shule kadhaa kuzuia wanafunzi kuhudhuria swala ya ijumaa.
Shule hizo zimepiga marufuku wanafunzi wote wa kiislamu kuhudhuri swala hiyo katika siku ya ijumaa kwa madai kwamba wanafunzi huchelewa kurudi shule na wengine hutumia fursa hiyo kwenda kula katika migahawa baada ya kufanya ibada hivyo kupelekea kuchelewa kurudi shule.
Wanafunzi wenye umri wa kuanzia miaka 10 ni lazima kwenda msikitini kuhudhuria swala ya Ijumaa kwa taratibu za shule za India.
Uamuzi huo umepingwa na wazazi kwa kuzitaka shule hizo ziruhusu vijana wao waendelee kuhudhuria swala ya ijumaa kama kawaida.
Aidha, wamewataka viongozi wa shule hizo kuhakikisha wanafunzi wanarudi katika muda uliopangwa na si kuwazuia kwenda msikiti. Baadhi ya shule zimeanza kuruhusu wanafunzi kuhudhuria swala ya ijumaa.
kati ya watu bilioni 1.1 nchini India, waislamu ni 160 milioni ambapo India ni nchi ya tatu kuwa na waislamu wengi duniani baada ya Indonesia na Pakistan.
CHANZO:AHBAABUR

wanafunzi wakiwa darasani |
About Omari Makoo
0 comments :
Post a Comment