-->

TUNU YA UKEREWE


 Image result for TUNU YAUKEREWE
TUNU YA UKEREWE
Na Omari Abdallah Makoo
Wilaya ya Ukerewe ni wilaya mojawapo ya Mkoa wa Mwanza. Katika sensa ya mwaka 2002, idadi ya wakazi wa wilaya hiyo ilihesabiwa kuwa 261,944
Eneo la wilaya hii liko kwenye visiwa ndani ya ziwa Viktoria .
Mmoja ya wapigania uhuru wa Tanganyika Hamza Mwapachu aliwahi kupelekwa wilaya ya Ukerewe ikiwa kama njia ya kumtenganisha na wapigania uhuru wenzake wakina Dr Kyaruzi,Nyerere pamoja na Sykes.
Hamza Mwapachu alipelekwa "uhamishoni" Kisiwa cha Ukerewe, kilichopo katikati ya Ziwa Viktoria. Dk. Kyaruzi aliutafsiri uhamisho huo kama "kifungo chenye sura iliyojificha".
Hamza Mwapachu alikuwa miongoni mwa wanafunzi walioanzisha umoja wa kutetea haki za wanafunzi wanaosoma Makerere Uganda wakitokea Tanganyika.
Umoja ule ulianzishwa na watu watatu Mwl Nyerere,Hamza Mwapachu pamoja na mwanafunzi ambaye aliwatangulia mwaka mmoja wakina Hamza mwapachu aliyefahamika kama Andrew Tibandebage.
Katika miaka ya zamani Ukerewe ilikuwa ikitawaliwa na watemi kama vile Mtemi Gabriel Ruhumbika,Mtemi Michael Rumbukizya na wengine wengi.
Wilaya hii ya Ukerewe inakumbukwa kwa kutoa Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kati ya mwaka 1991-1994,ambaye pia alikuja kuchaguliwa kuwa spika wa bunge kuanzia mwaka 2000 mpaka 2005.
Pia Peter DM Bwimbo ambaye alikuwa Mlinzi Mkuu wa Mwalimu Nyerere naye pia ni mtu wa kutokea Ukerewe.
Wkazi wa Ukerewe hawaui nyoka aina ya chatu kutokana na historia ya mmoja ya watawala(mtemi) wao kufuga chatu ambaye aliaminika kama mlinzi wa mtemi huyo.Hivyo baada ya hapo ni mwiko kuuwa chatu ukerewe na ukiua basi itabidi ukipata mtoto umwite Lusato au nyasato la sivyo ataugua na kufa au wewe mwenye kupata madhara.
Pia Ukerewe hawali ndege wanaoitwa nfunzi wakiamini kwamba ukila ndege huyo utaugua ugonjwa wa kuvuka ngozi ya juu na ngozi ya ndani kuja juu.Lakini hekima ya kutoliwa ndege hao inasemekana kuwa ni ndege ambao walikuwa wanatumika na waganga wa kienyeji kama dawa hivyo walizuiwa kuliwa ili wasije wakapotea wakakosa dawa.
Kingine ni darubuni ya asili inayopatikana katika mapango ya Handebezyo ni vilima vitano ambavyo chini yake kuna mapango, katika eneo la Makumbusho ya Utawala wa Kikerewe. Wenyeji wa Visiwa hivi wanasema ‘Handebezyo’ maana yake ni ‘Sehemu ya kuchungulia’.

Ukiwa katika eneo hili unaweza kuona mipaka yote ya Kisiwa cha Ukerewe na visiwa vingine vinavyozunguka eneo hili vikiwamo Visiwa vya Ilugwa na Kulazu vilivyoko mashariki vikipakana na wilaya ya Musoma mkoani Mara, unaweza kuona Kisiwa cha Ukara na hata sehemu ya Jiji la Mwanza.

Inadaiwa kuwa miaka mingi iliyopita vilima na mapango haya yalitumika kama ngome ya vita dhidi ya wakoloni na vita baina dhidi ya makabila ama falme nyingine.

Wazee wa Kabila la Wakerewe walilitumia kama ‘darubini’ yao kwani walipanda juu ya vilima vya Handebezyo na kuangaliaa iwapo kulikuwa na viashiria vya hatari ama wavamizi wanaokuja, hivyo kujiandaa kupambana nao. Mapango yalitumika kama sehemu ya kujificha dhidi ya maadui.
Kingine ni jiwe linalocheza ambalo linafahamika kwa jina la Nyaburebheka lililopo kisiwani Ukara.Jiwe hilo linasemakana huwa linacheza baada ya kufanyiwa mambo ya kimila na koo inayomiliki jiwe hilo ambalo kwa sasa amerithishwa kijana aitwae Mtari
Karibu Ukerewe uje ujionee mengi
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment