Kwa mujibu wa waandishi na watafiti mbalimbali, mfano Sengo (1975), Kezilahabi (1976) na Gibbe (1980) wanasema kuwa jumla ya kazi alizowahi kuzitunga Marehemu Sheikh Shaaban Robert na zilizochapishwa hadi sasa ni ishirini na mbili, ambapo kumi na nne ni za ushairi na nane ni za nathari. Hata hivyo baadhi ya maandiko ya watafiti wa hivi karibuni mfano Mulokozi (2002) na Chuachua (2008) yanaonesha kuwa jumla ya maandiko ya Sheikh Shaaban Robert yaliyokwisha kuchapwa hadi hivi sasa ni ishirini na nne.
Ponera (2010) anaungana na Mulokozi (2002) na Chuachua (2008) kwa kuorodhesha vitabu ishirini na nne vya Sheikh Shaaban Robert vikiwa kumi na nne ni vya ushairi na kumi ni vya nathari.
Ponera (2010) anavitaja vitabu hivyo vya ushairi kuwa ni:
1) MWAFRIKA AIMBA (1969), Nelson. Nairobi
2) ALMASI ZA AFRIKA (1971), Nelson, Nairobi
3) KOJA LA LUGHA (1969), Oxford, Nairobi
4) INSHA NA MASHAIRI (1967), Nelson, Nairobi
5) ASHIKI KITABU HIKI (1968), Nelson, Nairobi
6) PAMBO LA LUGHA (1968), Oxford, Nairobi
7) KIELEZO CHA FASILI (1962), Nelson, Nairobi
8) MASOMO YENYE ADILI (1959), Art&Literature, Nairobi
9) MAPENZI BORA (1969), Nelson, Nairobi
10) TENZI ZA MARUDI MEMA NA OMAR KHAYYAM (1973), TPH, Dar-es- salaam
11) UTENZI WA VITA VYA UHURU (1961), Oxford, Nairobi
12) ALMASI ZA AFRIKA NA TAFSIRI YA KIINGEREZA (1960), Art&Literature, Nairobi
13) MASHAIRI YA SHAABAN ROBERT (1971), Nelson, Nairobi
14) SANAA YA USHAIRI (1972), Nelson, Nairobi.
Na vitabu vya nathari vya Sheikh Shaaban Robert ni:
15) KUFIKIRIKA (1968),Oxford, Nairobi
16) WASIFU WA SITI BINTI SAAD (1967), Art&Literature, Nairobi
17) MAISHA YANGU NA BAADA YA MIAKA HAMSINI (1949), Nelson, Nairobi
18) KUSADIKIKA (1951), Nelson, Nairobi
19) ADILI NA NDUGUZE (1977), TPH, Dar-es- salaam
20) UTU BORA MKULIMA (1968), Nelson, Nairobi
21) SIKU YA WATENZI WOTE (1968), Nelson, Nairobi
22) KIELELEZO CHA INSHA (1954), Witwatersand, Nairobi
23) BARUA ZA SHAABAN ROBERT 1931- 1958, (2002), TUKI, Dar- es- salaam 24) MITHALI NA MIFANO YA KISWAHILI (2007), TUKI, Dar-es- salaam.
MAREJELEO
Sengo,T. S. Y (1973), SHAABAN ROBERT: UHAKIKI WA MAANDISHI YAKE. Longman; Dsm
Kezilahabi, E (1976), USHAIRI WA SHAABAN ROBERT. EALB Nairobi
Gibbe, A. G (1980), SHAABAN ROBERT; MSHAIRI.TPH. Dsm
Mulokozi, M. M (2002) BARUA ZA SHAABAN ROBERT 1931-1958. TUKI. Dsm
Chuachua, R (2009) NAFASI YA MWANAMKE KATIKA NATHARI ZA SHAABAN ROBERT: Ripoti ya Utafiti Chuo Kikuu cha Waislam (Haijachapwa)
Ponera, A (2010) ATHARI ZA UFUTUHI KATIKA NATHARI ZA SHAABAN ROBERT Tasnifu ya Uzamili Chuo Kikuu cha Dodoma
……………………………….
Post hii imeandikwa na Mbwana Rashid Cameroo Allyamtu lakini ni utafiti uliofanywa na Dkt Hassan Hassan ambaye ni Mwalimu na Mtaalamu wa Lugha ya Kiswahili (Isimu&Fasihi). Pia ni mtunzi wa mashairi, mhakiki na mhariri.
...................................................

0 comments :
Post a Comment