Aliko
Dangote, mtu tajiri zaidi barani Afrika,ana mpango wa kuinunua klabu ya
Arsenal kutoka nchini Uingereza katika kipindi cha miaka minne.
Dangote
ambaye ni raia wa Nigeria ana thamani ya dola bilioni 10.9,kulingana na
orodha ya watu tajiri duniani iliotolewa na runinga ya Bloomberg mjini
New York siku ya Jumatano, alitangaza nia yake ya kukinunua klabu hicho
mwaka uliopita.
Alisema
kuwa anasubiri biashara zake kuimarika pamoja na uwekezaji wake wa
ujenzi wa bomba la gesi na kiwanda cha kusafisha mafuta kabla ya
kukinunua klabu hicho.
''Hakuna tatizo kwamba nitainunua klabu hiyo, na si tatizo la fedha," alisema Dangote katika mahojiano na runinga ya Bloomberg .
''Pengine
miaka mitatu au mine. Suala ni kwamba tuna changamoto nyingi.
Ninahitajika kukabiliana nazo mwanzo baadaye nitaangazia suala la
ununuzi huo''.
Dangote
ambaye ni shabiki mkubwa wa Arsenal amepoteza kiasi cha dola bilioni
4.4 mwaka huu kutokana na kushuka kwa thamani ya sarufi ya Nigeria.
Utajiri wake mwingi upo katika kiwanda cha saruji kilichopo mjini Lagos.
Iwapo atainunua timu hiyo basi atakuwa mtu wa kwanza kutoka barani Afrika kumiliki timu iliyopo katika Ligi Kuu ya England
CHANZO:MPENJA SPORTS
0 comments :
Post a Comment