WAKATI ripoti ya kamati iliyoundwa na
serikali kuchunguza tuhuma za vigogo walioficha fedha kwenye mabenki ya
nje ya nchi ikiwa bado haijatolewa bungeni, Mbunge wa Kigoma Kaskazini,
Zitto Kabwe (CHADEMA), amewataja vigogo watatu kuwa miongoni mwa
wahusika.
Zitto ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA (Bara), ndiye muasisi wa hoja hiyo bungeni. Hivi karibuni alitishia kuwataja wahusika endapo serikali haitawasilisha ripoti hiyo kwenye mkutano wa Bunge uliomalizika Jumamosi.
Mbunge huyo aliwataja vigogo hao juzi wilayani Kaliua mkoani Tabora wakati akihutubia maelfu ya wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Kolimba.
Bila kutaja majina yao, Zitto aliwataja kwa nyadhifa zao walizowahi kushika akisema ni aliyewahi kuwa Waziri wa Nishati na Madini, Waziri wa Ulinzi wa zamani na aliyewahi kuwa mkuu wa majeshi.
Alisema baada ya kutoa hoja bungeni ya kuitaka serikali ifanye uchunguzi juu ya Watanzania walioficha fedha nje ya nchi, alichaguliwa kuongoza timu ya kufuatilia sakata hilo, kupitia taasisi ya Eurodad, ambapo alifanya ziara katika sehemu mbalimbali ikiwemo nchini Uswisi na Uingereza.
Zitto alifafanua kuwa akiwa huko alikutana na wadau mbalimbali wa masuala ya kibenki pamoja na kuhudhuria mkutano wa Waziri Mkuu wa Uingereza uliokuwa ukizungumzia utoroshwaji wa fedha.
“Hawa watu wanajulikana na tutawataja kwa majina mchakato ukikamilika, lakini kwa sasa niwaambie miongoni mwa watu hao ni pamoja na waliowahi kuwa mawaziri na mmoja wa wakuu wa majeshi mstaafu,” alisema Zitto.
Alisema kutokana na hali hiyo, serikali inaendelea kushikwa na kigugumizi cha kuwaanika watu hao hadharani licha ya Serikali ya Uswisi kuitaka isaini mkataba wa kubadilishana taarifa.
Zitto alisema kwa sasa ameshawaagiza wasaidizi wake katika masuala ya kibunge kuandika utaratibu utakaowasilishwa bungeni kwa ajili ya kuwadhibiti watu wanaoficha fedha nje bila kuwa na maelezo ya kutosha.
Aliongeza kuwa suala la kuwaanika hadharani watu wanaoficha fedha nje ya nchi linahitaji uungwaji mkono wa hali ya juu kwa kuwa ni kazi ya hatari inayowagusa watu wenye maslahi na uwezo mkubwa nchini.
Kwa mujibu wa mbunge huyo, mbali na Tanzania, nchi nyingi za Afrika zinaweka fedha nyingi Uingereza pamoja na visiwa vyake 15 ambapo katika kisiwa cha Jersey pekee kuna paundi bilioni 40 za Uingereza.
Zitto alisema baadhi ya nchi huwafilisi watu ambao wanabainika kuwa wameficha fedha nje na kuzitumia kwa shughuli mbalimbali za kijamii.
Alisema kuwa wakati anafanya shughuli hiyo aliyosema ni ajenda ya kitaifa, alitegemea kuungwa mkono na watu wake wa karibu, ikiwa ni pamoja na walio ndani ya chama chake.
“Hivi ni vita visivyohitaji utengano, tunapoamua kulumbana sisi kwa sisi wenzetu wanapata mwanya wa kufanya mambo yao, nilitegemea katika hali hii CHADEMA tushikamane kuliangamiza hili dude CCM,” alisema Zitto.
Kuhusu migogoro
Zitto alisema CHADEMA hawama migogoro na kinachofanyika ni mikakati ya watu wachachahe wasio na shughuli kuamua kuwagonganisha viongozi.
“Kuna watu wachache sana ambao hawana kazi, shughuli yao ni kugonganisha viongozi ili wagombane na ikitokea hivyo wao ndiyo furaha kwao, sio ufahari hata kidogo kwa CHADEMA kuonekana ina migogoro,” alisema.

0 comments :
Post a Comment