Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imepanga kuanza kusikiliza maombi ya marejeo yaliyowasilishwa na Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Issa Ponda.
Sheikh Ponda aliwasilisha maombi hayo baada
kutoridhika na uamuzi uliotolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro wa
kukataa ombi lake la kulifuta shitaka la kuwa yeye alivunja masharti ya
kifungo cha nje kilichotolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Mei 9,
mwaka 2013.
Hukumu hiyo ilikuwa ikitamka awe akihubiri amani.
Kwa mujibu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro,
jalada la kesi hiyo, lilipelekwa katika Mahakama Kuu tangu Oktoba mwaka
huu na kwa upande wao itakuwa ikitajwa wakati wakisubiri matokeo ya
Mhakama Kuu.
Kesi ilikuwa katika hatua ya kuanza kusikilizwa kwa upande wa mashtaka kupeleka mashahidi wao.
Katika kesi hiyo, inayoendeshwa na Wakili wa
Serikali Mwandamizi, Benard Kongola na kusikilizwa na Hakimu Richard
Kabate , Sheikh Ponda anadaiwa kutenda makosa ya uchochezi Agosti 10,
mwaka 2013.
Inadaiwa kuwa alifanya hivyo katika maeneo ya Kiwanja cha Ndege cha Morogoro.
Inadaiwa kuwa Sheikh Ponda alialikwa kutoa maelezo
machache kwenye Kongamano la Eid lililoandaliwa na Umoja wa Wahadhiri
wa Mkoa wa Morogoro (Uwamo).
Inadaiwa kuwa akiwa hapo alitamka maneno: “Ndugu
Waislamu, msikubali uundwaji wa kamati za ulinzi na usalama za misikiti
kwani kamati hizo zimeundwa na Baraza la Waislamu Tanzania (Bakwata),
ambao ni vibaraka wa CCM na Serikali na kama watajitokeza kwenu watu hao
na kujitambulisha kwamba wao ni kamati za ulinzi na usalama za
misikiti, fungeni milango na madirisha ya misikiti yenu na muwapige
sana.”
Mamlaka ya Serikali zinadai kuwa maneno hayo ni ya uchochezi na ni kosa kisheria.
Pia Sheikh Ponda anadaiwa kuwashawishi wafuasi
wake kutenda kosa la jinai kwa kuwaambia: Serikali ilipeleka Jeshi
Mtwara kushughulikia suala la vurugu iliyotokana na gesi kwa kuwaua,
kuwabaka na kuwatesa wananchi kwa sababu asilimia 90 ya wakazi wake ni
Waislamu.
0 comments :
Post a Comment