MWANASHERIA Mkuu wa Chama Cha Demokrasia
na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu ameshindwa kujibu maswali ya
waandishi wa habari kuhusu suala la Kamati ya Bunge ya Hesabu za
Mashirika ya Umma (PAC), ambayo Zitto alidai kwamba Chama hicho
kimemtuhumu kuwa amekidhalilisha chama kwa tamko la PAC ,kwamba Hesabu
za Vyama vya Siasa ikiwemo Chadema hazijakaguliwa na Mdhibiti na Mkaguzi
Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).
Lissu alisema kwamba, hawawezi kuzungumzia suala la PAC wakati kuna jambo zito ambalo watuhumiwa hao walipanga kulifanya ndani ya Chama,"Hatuwezi kupoteza muda kujadili suala la PAC, wakati watuhumiwa hao walikuwa na lengo la kufanya mapinduzi ndani ya Chama, ndiyo maana tuliamua kufanyia kazi suala la mapinduzi yao ndani ya Chama na si suala la PAC" alisema Lissu
Mbunge wa Jimbo la Ubungo John Mnyika akizungumza na waandishi wa habari katika Ofisi za Makao Makuu ya Chadema,Kinondoni jijini Dar es Salaam,kulia ni Mwanasheria Mkuu wa Chama hicho Tundu Lissu.
Lisu akaongeza
"Ukweli ni kwamba suala la PAC halina hoja ya msingi katika suala hili kwa sababu si kazi ya vyama vya Siasa ikiwemo Chadema kujua ni kwanini hazijakaguliwa hili si suala la Zitto wala si suala la vyama vya siasa, bali ni suala la Ofisi ya CAG kujua kuwa vyama gani havijawasilisha mahesabu yao kwa ajili ya ukaguzi,tuliwahi kumkatalia CAG kwamba, hatuwezi kulipia garama za kukaguliwa kwa sababu hiyo ni kazi ya serikali na ofisi ya CAG ndiyo inapaswa kulipia garama hizo".
Kuhusu suala la Zitto kutuhumiwa katika mapinduzi ndani ya Chama, Lissu alisema,;"Zitto anatafuta pakukimbilia ila ukweli ni kwamba amefukuzwa ndani ya Chama, yeye pamoja na washirika wake kwa sababu ya waraka huu na tayari wameshapewa hati zao za mashtka yenye tuhuma 11,wakisha zijibu ni kwanini wasifukuzwe kabisa ndani ya Chama,wataitwa mbele ya Kamati Kuu kwa ajili ya hatua za mwisho".
Kauli za kujirudia rudia za Tundu Lissu ambaye ni Mwanasheria wa Chadema, kuhusu Zitto kufukuzwa ndani ya Chama ni ishara kwamba tayari Chama hicho kina nakala ya hukumu ya Zitto na ndiyo maana wameamua kutangaza mchakato wa Uchaguzi Mkuu wa Chama, wakiwa na uhakika kwamba hataweza kugombea nafasi yeyote katika Uchaguzi huo ikiwa ni tofauti na inavyo fahamika kwamba Zitto amevuliwa vyeo vyake vyote.

Source: HABARIMPYA
Blogger Comment
Facebook Comment