Habari. Leo ningependa kutoa maelekezo ya jinsi ya kuanzisha blog kwa
kutumia blogger. Kama hujawahi kua mtumiaji wa blogger basi maelezo haya
machache yatakua msaada kwako.
UNAHITAJI NINI?
Ili uweze kufungua blog kwa kutumia blogger unatakiwa uwe na akaunti ya google. Kama wewe ulishawahi kua na E-Mail ya Gmail, akaunti ya You Tube au ulishawahi kushiriki katika magroup ya google basi hutakua na haja ya kufungua akaunti ya google.
Unachotakiwa kufanya ni kuingia blogger.com na tumia email na neno lako la siri kuingia. Kama huna akaunti ya google ingia hapa na utengeneze akaunti mpya.
Kama una akaunti ya google au kwa aliyeisha maliza kutengeneza akaunti utakutana na kitu kama hiki. Ambapo utatakiwa uchagua kichwa (Title) ya blog yako
Muhimu: Chagua kichwa (title) kinachoendana na kile unachokiandika katika blog yako au unaweza tumia japo maneno mawili ambayo yanaendana na unachokiandika katika blog yako. Hii itakusaidia pale mtu anapotafuta blog yako katika Search Engine kama Google, Yahoo, Bing n.k kwa urahisi zaidi. Mfano mzuri ni blog ya blog hii ya BUSTANI YA HABARI unaweza kuona kuwa blog ina Title hii ‘’BUSTANI YA HABARI’’. Kwa hiyo mtu anaposearch jina Dj Choka ni rahisi sana kuipata blog yake.
Hatua inayofata ni kuchagua Template(mwonekano wa blog) ya kuanzia, ieleweke kwamba katika hatua hii unatakiwa kuchagua template unayoona inakufaa. KUhusu mwonekano wa template hiyo usikupe mawazo sana kwani baadae unaweza kuubadilisha na kuufanya vile upendavyo.
Hatua ya mwisho unayotakiwa kufanya ni kubofya(click) button ya rangi ya chungwa iliyoandikwa ‘’Create Blog’’ na baada ya hapo blog yako itakua tayari kwa kuwekwa habari. Kumbuka kama una swali lolote linalokutatiza kuhusu hatua za ufunguaji wa blog mpya usisite kuandika shida yako hapo chini au kuweka maoni yako
CHANZO:BONGOCLAN

0 comments :
Post a Comment