-->

MAMIA YA WATU WAJITOKEZA KUMZIKA SHEKH MUHIDIN BIN ABDULRAHMAN AL'ZINJIBAR



Mamia ya wakazi wa Unguja juzi wamejitokeza kumzika Sheikh Muhidin Bin Abdulrahman Al'zinjibar huko katika makaburi ya mwanakwerekwe,Unguja visiwani Zanzibar.

Sheikh Muhidin Bin Abdulrahman Al'zinjibar alifariki usiku wa jumanne wa tarehe 12/11/2003 Nyumbani kwake Zanzibar. Mazishi yake yalitawaliwa sana na Dua, nyiradi na dhikri mbalimbali.

Sheikh Muhidin Bin Abdulrahman Al'zinjibar anatajwa kama ndiye mjuzi Taarikhe za Tariqa za Ki-Sufi kwa Zama hizi. Na alikuwa Msomi na mwenye adabu za dini.

Sheikh alikuwa akiishi kuwait na kufanya kazi huko. Aliondoka kuwait mwaka 1992 na kwenda UAE,Dubai. Kuja kwake Tanzania kulitokana na ukaribu wake na Sheikh
Ar rifai.

Aidha katika uhai wake alikusanya vitabu vingi vya nyiradi vikiwemo 'man-baul amdaad' na 'fil adhkaar wal awraad'. Tunamuombea kwa Mwenyezi Mungu amsamehe makosa yake na amuingize katika pepo ya juu,aamin





Al marhum Sheikh Muhidin Abdulrahman
Waumini waliojitokeza kumzika Sheikh Muhidin abdulrahman       
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment