-->

IDADI YA TEMBO WALIOULIWA KWA USHAHIDI WA KONTENA LILILOKAMATWA ZANZIBAR NI 510

Shehena ya meno ya tembo yaliyokamatwa juzi katika Bandari ya Zanzibar ni ya mamia ya tembo wapatao 510 na thamani yake ni Sh. bilioni 7.4. Jeshi la Polisi Zanzibar limesema kuwa Kampuni ya Island Sea Shelts Limited iliyopo visiwani humo ndiyo mmiliki wa kontena lililokuwa limesheheni magunia 95 yenye meno 1,021 ya tembo meno sawa na tembo 510 kwa vile kila tembo ana meno mawali. Shehena hiyo ilikuwa inapelekwa china kupitia hong kong.

Wakati haya zanzibar yakiwa bado mabichi huko Katavi hakimu wa mahakama mkoani hapo amewahukumu wachina wawili kwenda jela miaka 70 kwa kukutwa na meno ya tembo yenye thamani ya
tsh millioni 45.
 HAWA NAO NI WALE WALIOKAMATWA WIKI MOJA KABLA YA TUKIO LA KUKAMATWA KONTENA 
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABALI HII HAPO CHINI
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment