-->

SHUHUDIA PICHA ZA KIJANA ALIYENUSURIKA KUFA BAADA YA KUTUHUMIWA KUWA NI MWIZI


Kijana mmoja asiyejulikana jina,amenusurika kifo baada ya kupata kipigo kikali kutoka kwa waumini wenye hasira.

Mkasa huo wa kusikitisha ulitokea jana baada ya swala ya adhuhuri katika moja ya misikiti iliopo katikati ya jiji la Dar es salaam.

Kamera ya munira blog ilimshhudia kijana huyo akiwa kapasuliwa vibaya sehemu za kichwani na usoni na kuusanya uso wake utapakae damu.

Huku akilia kwa uchungu kijana huyo alisikika akisema,sijawahi kuiba,sikuwa na lengo la kuiba na wala sitarajii kuiba,leo wema wangu umeniponza innaa lillaah wainnaa ilayhi rajiun.

Kwa mujbu wa mashuhuda wa tukio hilo walisema mara baada ya swala ya adhuhuri kijana huyo akiwa anatoka msikitini aliukuta mfuko wa viatu ukiwa katika mazingira mabaya ya kukanyagwa naye akaona aokote ili auweke pembeni.

Wakati anainama kwa lengo hilo mwenye mfuko wa viatu alimuona na kuanza kumuitia mwizi na watu kumshambulia.

Kwa kweli huyu kijana si mwizi,bali watu wamechukulia jazba,jambo hili si sahihi katika uislamu alisikika muumini mmoja aliyeshuhudia tukia zima.

Kumekuwa na wimbi la kuchukua sheria mkononi pasipo hatia kitu ambacho licha ya kusababisha ulemavu na vifo kadhaa lakini ni kinyume cha mafundisho sahihi ya Uislamu.




CHANZO:MUNIRA MADRASA
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment