-->

JIFUNZE NAMNA YA KUJIZUA NA MDOMO KUTOA HARUFU MBAYA


Harufu mbaya mdomoni inachagizwa na mambo kadhaa ikiwamo tabia zetu za kila siku na maradhi ya meno. Wakati mwingine jambo hili laweza kukufanya ushindwe kujiamini wakati wa kuzungumza na watu. Lakini pia laweza kuwafanya wanaokuzunguka wakushushe thamani wakidhani wewe ni mchafu...na kumbe una maradhi.


Tatizo la kunuka mdomo linawapata baadhi ya watu, ambao hata wakipiga mswaki, lakini bado ananuka mdomo hata pale anapotumia vitu vya kuufanya mdomo unukie vizuri kama ‘Chewing gum’ pipi hususan pipi-kifua na hata Big G bado mtu mwenye tatizo hilo ataendelea kuwa naMharufu mbaya.


Wanasayansi wamekiri kwamba ni vigumu sana mtu kufahamu kuwa ana harufu mbaya kwa sababu ya mazoea lakini ni
rahisi sana kutambua harufu kutoka kwenye kinywa cha mtu mwingine. Unaweza kutambua kama una harufu mbaya mdomoni kwa kumuuliza mtu unayemuamini na pia unaweza kujua
harufu mbaya kwa kulamba nyuma ya kiganja na kunusa, wengine hupumua mbele ya kioo na kunusa.

Pia unaweza kutumia kijiti cha kuchokonolea meno na kukinusa. Kisayansi unaweza kutumia vifaa kama ‘Halimeter’M‘Gas’ ‘Chromatography ‘na ‘BANA Test.

“Magonjwa ya kinywa yanasababishwa na mabaki ya chakula kwa kuwa mwili wa binadamu una vijidudu aina ya bacteria ambao kwa kitaalamu huitwa ‘normal flora’. Wadudu hao mara wanapokula hutoa tindikali ambayo husababisha magonjwa ya
fizi na kinywa.


Vitu vyenye sukari ikiwemo sukari ya kawaida pia huchochea tatizo hili, lakini mpangilio wa meno katika kinywa huhifadhi mabaki na kuleta harufu mbaya,” Anaeleza kuwa tatizo hili pia huchangiwa
na vijidudu vya ‘bacteria’ wanaojificha kati ya jino na jino na wengine kama ana jino lililotoboka vijidudu hivi hutumia nafasi ya
kujificha humo.

 
Lakini wale ambao wana tabia ya kulala mdomo wazi, tabaka la juu la ngozi ya mdomo huoza na kutoa harufu mbaya.
Unywaji Pombe: Unywaji wa pombe husababisha kiwango cha kabohaidreti kubaki mdomoni na kuoza hivyo kusababisha magonjwa ya fizi.


Chanzo kingine kikuu cha harufu mbaya ya kinywa ni pale ambapo chakula kingi kinabaki mdomoni hasa hasa nyama.
Utumiaji wa chakula chochote kitakachokaa ndani ya mfumo wa usagaji wa chakula kwa muda mrefu kitaanza kuoza, na siku zote nyama inapooza huanza kutoa harufu mbaya (kunuka ).

Kwa hiyo hiki nacho ni chanzo kikubwa cha harufu mbaya ya kinywa. Harufu hii ya mdomo inaanzia kwenye kinywa na kushuka kwenye mapafu na kusababisha tatizo hilo kuwa kubwa zaidi.
Nini cha kufanya unapokuwa na tatizo Hili:
Cha kufanya iwapo una tatizo la kutoa harufu kwenye kinywa hakikisha unapiga mswaki mara baada ya mlo. Ili kuwaondoa
vijidudu vya bacteria wanaotokana na mabaki ya chakula na pia kama unajino lililotoboka ni bora kuling’oa au kulitibu kwa
njia ya kusafisha meno na kujaza risasi,


Pia unaweza kutibu kwa njia mbadala kwa kutumia Ndulele ili kuondoa vijidudu vya bacteria vinavyotoboa jino wasiambukize
meno mengine. (Ndulele zinafanana na nyanya chungu lakini haziliwi). Wale ambao wakipiga mswaki damu zinatoka kwenye fizi, hiyo ni dalilia hatari.


Matibabu ya fizi
“Tatizo la Fizi (Non Communicable disease)
kama yalivyo mafua makali, kifua, koo na kisukari yanahitaji matibabu ya mara kwa mara. Ni vyema kusafisha meno kwa dawa na kupata elimu ya jinsi ya kuepukana na tatizo hili.


Wanawake wanaongoza
Wanawake ndio waathirika wakubwa wa tatizo la meno
kwani kati ya wagonjwa 10 ambao amekuwa akipata tiba kwa siku katika hospital ya Hurbet Kairuki Iliyopo Dar es salaam, saba ni
wanawake huku watoto wadogo wakifuatia kwa tatizo la kuvunjika meno kutokana na kula vitu vyenye sukari nyingi.


“Watoto hawanuki mdomo lakini wengi wanaokuja hapa wametoboka meno na wengine yamevunjika na hii inasababishwa
na mfumo wa maisha, wanapewa vyakula laini hawahitaji kutafuna sana, vyakula vya makopo, chipsi, na watoto kuanzia umri wa
miaka mitano hadi tisa ndio wanaongoza kwa tatizo hili,” anasema daktari moja katika hospitali ya KAIRUKI.


Ushauri aina ya vyakula vya kujiepusha na magonjwa ya meno, watu warudi kwenye vyakula vya asili kwani meno hujisafisha yenyewe.


Kupiga mswaki
Wengi wetu tumezoea kupiga mswaki asubuhi tu, lakini tunakula vitu vingi kutwa nzima na kisha kulala na mchanganyiko wa vyakula hivyo katika ulimi na meno.


Wataalamu wa afya wanasema, mtu anatakiwa kupiga mswaki mara tatu kwa siku asubuhi anapoamka, baada ya chakula
cha mchana na wakati wa kulala. Akiweza, apige mswaki kila baada ya mlo.


Magonjwa ya kinywa alisema kama tatizo linaanzia mdomoni ni vyema mgonjwa akatumia dawa maalumu ya kusukutua kinywa kwa muda maalumu ambayo itasaidia kuwaua bakteria
wanao sababisha harufu mbaya ya kinywa.


Lakini pia nashauri watu kutumia dawa maalumu ambayo itaenda kuondoa uchafu wote uliooza na uliogandamana
tumboni na kwenye mapafu ambao ndio chanzo cha kutokwa na harufu mbaya ya kinywa.


Tahadhari kwa vitu
vifuatavyo:

Epuka: Kula vyakula kama vitunguu maji, vitunguu swaumu, unywaji wa pombe, vyakula vyenye protini nyingi kama vile
samaki, matumizi ya sukari, kahawa na baadhi ya aina za dawa za mswaki.


“Pombe hukausha kinywa, Kinywa kikavu huchochea mazalio ya bakteria wanao sababisha harufu mbaya ya kinywa,”

Usivute sigara: “ Kama kweli mgonjwa ana nia ya kumaliza tatizo la kutokwa na harufu mbaya ya kinywa anapaswa kuachana na uvutaji wa sigara kwani sio tu unasababisha harufu mbaya ya kinywa bali pia utakausha kinywa chako na hivyo kusababisha mazalio ya bakteria wasababishao harufu mbaya ya kinywa.

Unywaji Kahawa: Kahawa ina tindikali ambayo husababisha kuzaliwa kwa bacteria wanaosababisha harufu mbaya
ya kinywa.


Zingatia: kunywa maji mengi kila siku angalau lita tano kwa siku, kwani kwa kufanya hivyo kutakusaidia kuosha chembechembe za vyakula ambavyo vimebaki mdomoni na vilevile usaidia kuepusha mdomo kuwa mkavu.


Pia watu kujenga utaratibu wa kuzifanyia uchunguzi afya zao
mara kwa mara sio tu ya kinywa bali ya mwili mzima kwa ujumla kwani kuna baadhi ya watu wananuka mdomo lakini
hawajitambui kama wana hilo tatizo lakini kwa kufanya hivyo watajitambua na kushauri angalau mara tatu kwa mwaka
kwa afya ya kinywa na mara moja kwa mwaka kwa afya ya mwili mzima.  

CHANZO:http://www.manyandahealthy.blogspot.com
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment