-->

ICC YAMTAKA RAISI KENYATA KUHUDHURIA MAHAKAMANI

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta na Naibu wake William Ruto ambao wanakabiliwa na mashtaka katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita ICCMahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) siku ya
Jumanne (tarehe 26 Novemba) iliubadili uamuzi
ambao ungelimruhusu Rais Uhuru Kenyatta
kuhudhuria sehemu ya kesi yake, badala yake
ikasema kwamba Kenyatta "kwa ujumla lazima
awepo mahakamani", liliripoti shirika la habari la
AFP.
"Maombi yoyote hapo baadaye ya kuruhusiwa
kutohudhuria sehemu ya kesi yake yatazingatiwa
kwa msingi wa kesi na kesi," ilisema mahakama
hiyo ya ICC yenye makao yake mjini The Hague
katika taarifa yake.
Siku ya tarehe 18 Oktoba, majaji walimruhusu
kwa sehemu fulani Kenyatta kutohudhuria kesi
zake ili ashughulike na matokeo ya kuzingirwa
kwa jengo la maduka la Westgate jijini Nairobi
na al-Shabaab mwezi Septemba ambako kiasi
cha watu 67 walikufa.
Majaji wa ICC siku ya Jumanne waliamua
kwamba kutokuwepo kwa Kenyatta
"kutaruhusiwa tu katika mazingira maalum na
lazima kuwe kwa yale tu ambayo ni ya lazima."
Mchimba Riziki
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment