-->

HAKIMU ASHINDWA KUFIKA MAHAKAMANI KATIKA KESI YA SHEKH PONDA KUTOKANA NA KUPATWA HOMA

Kesi ya shekh Ponda iliyokuwa inasomwa mara kadhaa mkoani morogro,hapo jana ilitakiwa kusikikilizwa jijini Dar es salaam katika mahakama kuu baada ya wakili wa shekh Ponda Bw. Nassoroanaesimamia kesi hiyo ya shekh Ponda kuomba faili la mteja wake kuhamishiwa Dar es salaam kwa hoja ya kwamba shtaka la tuhuma ya Shekh Ponda kutamka maneno ya kuhatarisha amani kinyume na masharti ya kifungo cha nje alichopewa katika mahakama kuu katika kesi ya kiwanja cha Markazi haina nguvu na pia anaamini mteja wake hana hatia na kosa hilo hilo aliomba dhamana katika mahakama ya hakimu mfawidhi mkoani mororgoro na ilipokuwa ngumu alifanya taratibu za kisheria mahakama kuu ili faili ya kesi hiyo ihamishiwe Dar es salaam,Hivyo tarehe 18/11/2013 ya jana kesi hiyo ilitakiwa kusikilizwa katika mahakama kuu jijini Dar es salaam.
Kwa mujibu wa (GAZETI LA FAHAMU 19/11/2013 ukurasa wa 2)
Habari kutoka mahakama kuu zinaeleza kwamba jaji wa Rose Temba ,aliyepangiwa kusikiliza maombi ya shekh Ponda kupata homa.Msajili Projestus Kayoza alipanga usikilizaji uwe Desemba 2 huku akieleza DPP kuwasilisha hati ya majibu ya Shekh Ponda.Baada ya hapo Shekh Ponda akiona ipo haja,atawasilisha maelezo ya hoja ya upande wa mashtaka.Shekh Ponda ameomba mapitio ya uamuzi wa kuzuiwa kwa dhamana yake kutokana na pingamizi iliyowekwa kwa DPP.
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment