-->

FIFA YASOGEZA MBELE TAREHE YA KUMCHAGUA MCHEZAJI BORA WA DUNIA(TUZO ZA BALLON D' OR)

Cristiano Ronaldo sasa yupo katka nafasi nzuri ya kutwaa tuzo yake ya pili ya Ballon d’Or baada ya kufunga mabao matatu yaliyoipeleka Ureno kombe la dunia 2014.

Kwa mujibu wa Sporting Life, Ronaldo amemuondoa  Franck Ribery katika kilele cha listi ya wachezaji waliokuwa wakipewa nafasi kubwa ya kutwaa tuzo hiyo.
Pia imeripotiwa kwamba shirikisho la soka duniani FIFA limeongeza muda wa kupiga kura za kumchagua mshindi wa 2013 Ballon d’Or.  Uamuzi wa FIFA kuruhusu makocha na manahodha pamoja na waandishi kuwasilisha majina matatu ya Top 3 kabla ya Nov. 29 tofauti na mwanzo ilivyokuwa Nov. 15, limeleta maswali mengi kutoka kwa wadau wa soka kama ilivyoripotiwa na ESPN FC
Kwa mujibu wa makala moja  iliyoandikwa kwenye ESPN FC ,  Francesc Aguilar aliandika kwenye mtandao wa: Sina maneno tena. FIFA na wameongeza muda wa kupiga kura mpaka Nov. 29 2013. Mara ya kwanza viwango vya wachezaji katika michezo ya pili ya kufuzu kombe la dunia 2014 havikuwemo katika katika mchakato. Hilo halikuwa sawa kama nilivyo na mashaka juu ya uamuzi wa sasa.  FIFA inaharibu mchakato wa kura za Ballon d'Or kwa maamuzi ya namna hii. Huhitaji kuwa na akili nyingi sana kuona kwamba uamuzi wa kuongeza siku za kupiga kura unamnufaisha zaidi CR7." alisema mwandishi huyo wa kihispania.
Listi ya wachezaji 23 wanaowania Ballon d’Or itakatwa mpaka kufikia wachezaji watatu tu Dec. 9, kabla ya mshindi hajatangazwa mwakani huko Zurich. Imekuwa ikifahamika wazi kwamba Ronaldo, Ribery na Lionel Messi wataunda top 3, lakini Ribery alikuwa akipewa nafasi kubwa kutokana na mchango wake aliotoa katika mafanikio ya kutwaa makombe matatu ya Bayern msimu uliopita.
Winga huyo wa kifaransa mpaka sasa hajapoteza mechi akiwa na klabu yake msimu huu, na alikuwa na mchango mkubwa kuisaidia Ufaransa kupata nafasi ya kwenda 2014 World Cup
CHANZO:SHAFFIH DAUDA
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment