-->

MWANZILISHI WA CHAMA CHA NCCR-MAGEUZI DR MVUNGI APOKEWA NA MAELFU YA WATANZANIA

Mwili wa aliyekuwa Mjumbe wa Tume ya mabadiliko ya Katiba mpya na Mkurugenzi wa Katiba, Sheria na Haki za Binadamu wa NCCR-Mageuzi, Marehemu Dk. Sengondo Mvungi umewasili nchini kutoka Afrika Kusini.

Maelfu ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam bila kujali itikadi ya vyama vyao, ndugu jamaa na marafiki wa Marehemu dk. Sengondo Mvungi walifika uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere upande wa Mizigo na kuupokea mwili wa kiongozi huyo na mwana familia.

Mapokezi ya mwili wa Dk. Mvungi aliyefariki juzi kufuatia majeraha ya shambulizi la majambazi lililomkuta nyumbani kwake novemba 2 mwaka huu na kupeleka Nchini Afrika Kusini kwa Matibabu, yaliongozwa na Mkewe mama Anne Mvungi.

Viongozi wengine waliohudhuria ni pamoja na Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba mpya, Jaji na Waziri Mkuu Mstaafu, Joseph Sinde Warioba, Waziri wa Uchukuzi, Dk. Sengondo Mvungi, Mwenyekiti wa NCCR-Magezi, na wajumbe takriban wote wa tume ya mabadiliko ya Katiba mpya. Sanduku alilowekwa Dr Mvungi lilipambwa bendera ya Chama cha NNCR-Magezi likizungukwa na vijana waliovaa sare za bendara ya chama chama, kama ingekuwa CCM wangeitwa grrengurd au chadema wangeitwa redbrigadi.

Utulivu ulikuwa mkbwa huku askali waliovaa sare na wasiovaa sare walikuwa sehemu ya mamia walifika kumpokea shujaa huyo wa katiba, Dr mvungi atazikwa kwao huko moshi nov 18 kama ratiba itakwenda kama ilivyopangwa.
Mungu Ibariki Tanzania.
MWANZILISHI WA CHAMA CHA NCCR-MAGEUZI DR MVUNGI APOKEWA NA MAELFU YA WATANZANIA BILA KUJALI TOFAUTI ZAO ZA VYAMA, KWELI INASIKITISHA NA KUUMA SANA!!

Mwili wa aliyekuwa Mjumbe wa Tume ya mabadiliko ya Katiba mpya na Mkurugenzi wa Katiba, Sheria na Haki za Binadamu wa NCCR-Mageuzi, Marehemu Dk. Sengondo Mvungi umewasili nchini kutoka Afrika Kusini.

Maelfu ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam bila kujali itikadi ya vyama vyao, ndugu jamaa na marafiki wa Marehemu dk. Sengondo Mvungi walifika uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere upande wa Mizigo na kuupokea mwili wa kiongozi huyo na mwana familia.

Mapokezi ya mwili wa Dk. Mvungi aliyefariki juzi kufuatia majeraha ya shambulizi la majambazi lililomkuta nyumbani kwake novemba 2 mwaka huu na kupeleka Nchini Afrika Kusini kwa Matibabu, yaliongozwa na Mkewe mama Anne Mvungi.

Viongozi wengine waliohudhuria ni pamoja na Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba mpya, Jaji na Waziri Mkuu Mstaafu, Joseph Sinde Warioba, Waziri wa Uchukuzi, Dk. Sengondo Mvungi, Mwenyekiti wa NCCR-Magezi, na wajumbe takriban wote wa tume ya mabadiliko ya Katiba mpya. Sanduku alilowekwa Dr Mvungi lilipambwa  bendera ya Chama cha NNCR-Magezi likizungukwa na vijana waliovaa sare za bendara ya chama chama, kama ingekuwa CCM wangeitwa grrengurd au chadema wangeitwa redbrigadi.

Utulivu ulikuwa mkbwa huku askali waliovaa sare na wasiovaa sare walikuwa sehemu ya mamia walifika kumpokea shujaa huyo wa katiba, Dr mvungi atazikwa kwao huko moshi nov 18 kama ratiba itakwenda kama ilivyopangwa.
Mungu Ibariki Tanzania.
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment